JOB Ndugai, Spika wa Bunge la Tanzania amevitaka vyombo vya dola nchini humo kutoa haraka taarifa za awali za uchunguzi wa tukio la kushambuliwa kwa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea)
Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo Jumanne tarehe 9 Juni 2020 bungeni jijini Dodoma, wakati akiwaeleza wabunge hali ya Mbowe baada ya kutoka kumwona katika Hospitali aliyokuwa amelazwa kabla ya kuhamishiwa jijini Dar es Salaam kwa matibabu.
Amesema, wakati anakwenda kumwona, amemkuta Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema akinywa chai na hali yake inaendelea vizuri huku akisema, hawezi kuongea zaidi kuhusu tukio hilo kwa madai lina mazingira yenye utata yanayoweza kuwekwa wazi na polisi.
Spika Ndugai amevitaka vyombo vya dola kuharakisha kutoa taarifa za uchunguzi wa tukio hilo ili kuepuka kuzusha maneno yasiyokuwa na maana kuhusu tukio hilo, “vyombo vya ulinzi na usalama vitoke mapema viseme nini kimetokea.”
“Naamini kesho (Jumatano) jioni saizi, nitakuwa na kiasi fulani cha kusema,” amesema Spika Ndugai
Akiendelea kuzungumza, Spika Ndugai amesema, hali ya usalama Dodoma haujatetereka.
“Niwahakikishie waheshimiwa wabunge, Dodoma ni salama, salama kabisa kabisa. Mmekaa hapa toka Aprili mwanzoni hadi sasa, hakuna aliyepoteza sikio, jicho, aliyechomoka mkono au kidole. Dodoma ni salama,” amesema Spika Ndugai
SALAMA KWA WALIO SHIKA MPINI AU SIO?