Job Ndugai, Spika wa Bunge la Tanzania

Spika Ndugai: Bunge Tanzania kuvunjwa Juni 19

Spread the love

SHUGHULI za Bunge la 11 nchini Tanzania, zinatarajiwa kuhitimishwa rasmi tarehe 19 Juni 2020 kwa Rais John Magufuli kulihutubia. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumatatu tarehe 18 Mei, 2020, na Spika Job Ndugai, wakati anazungumza na wanahabari jijini Dodoma kuhusu maazimio ya kikao cha Kamati ya Uongozi wa Bunge, kuhusu tathimini ya shughuli za mhimili huo.

“Pia niwajulishe, tumemaliza muda si mrefu kikao cha kamati ya uongozi wa Bunge, ambapo tulikuwa tunatahimini shughuli zetu. Tumekubaliana tumalize shughuli za bunge la 11 tarehe  19 Juni 2020, panapo majaliwa Rais Magufuli anaweza kuja kufunga rasmi,” amesema Spika Ndugai.

Awali, uongozi wa bunge ulitangaza kwamba, shughuli za mhimili huo uliozinduliwa tarehe 20 Novemba 2015 na Rais Magufuli zitafikia tamati tarehe 29 Mei 2020.

Lakini Spika Ndugai amesema mabadiliko ya ratiba hiyo, yametokana na mabadiliko katika vikao vya mabunge ya nchi za Afrika Mashariki.

Amesema, nchi za Afrika Mashariki zina desturi ya kusoma bajeti zao siku moja, mawaziri wa fedha wa nchi husika wamekubaliana kusoma bajeti zao tarehe 11 Juni, 2020.

Hivyo, Bbunge la Tanzania limeamua kughairisha kuhitimisha Bunge mwezi tarehe 29 Mei, 2020 ili liende sambamba na nchi hizo.

“Ratiba ya mwanzo haikuwa inaonyesha hivyo, badiliko ni kutokana na kwamba tuna tamaduni ya bajeti za bunge la nchi za Afrika Mashariki kusomwa pamoja. Lakini kutokana na janga la Corona, mawaziri wa fedha wamekubaliana tarehe 11 Juni isomwe bajeti, “ amesema Spika Ndugai.

SHUGHULI za Bunge la 11 nchini Tanzania, zinatarajiwa kuhitimishwa rasmi tarehe 19 Juni 2020 kwa Rais John Magufuli kulihutubia. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea). Taarifa hiyo imetolewa leo Jumatatu tarehe 18 Mei, 2020, na Spika Job Ndugai, wakati anazungumza na wanahabari jijini Dodoma kuhusu maazimio ya kikao cha Kamati ya Uongozi wa Bunge, kuhusu tathimini ya shughuli za mhimili huo. “Pia niwajulishe, tumemaliza muda si mrefu kikao cha kamati ya uongozi wa Bunge, ambapo tulikuwa tunatahimini shughuli zetu. Tumekubaliana tumalize shughuli za bunge la 11 tarehe  19 Juni 2020, panapo majaliwa Rais Magufuli anaweza kuja kufunga rasmi,” amesema Spika Ndugai. Awali, uongozi…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!