Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Spika Ndugai apora gari la Mbowe
Habari za SiasaTangulizi

Spika Ndugai apora gari la Mbowe

Freeman Mbowe, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni. Picha ndogo Spika Job Ndugai
Spread the love

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Bunge la Tanzania limeamuru kurudishwa nchini gari linalosaidia kumhudumia Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) aliyelazwa nchini Kenya akipatiwa matibabu ya majeraha ya risasi aliyoyapata aliposhambuliwa na watu wasiojulikana mjini Dodoma Sptemba 7 mwaka huu, anaandika Mwandishi Wetu.

Gari hilo linatumiwa na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe ambaye yupo jijini Nairobi nchini Kenya akimuuguza Lissu tangu alipofikishwa hospitalini hapo akiwa mahututi.

Mbowe anatumia gari hilo kama haki yake kwa mujibu taratibu zilizowekwa ambazo zinasema kiongozi wa kambi ya upinzani anatakiwa kupatiwa usafiri pamoja na dereva.

Lakini Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini Kenya, dereva wa gari leo la serikali aliamuliwa kulirudisha nyumbani na kumuacha bosi ambaye ni Mbowe bila usafiri.

Imedaiwa kuwa gari hilo ambalo analitumia Mbowe lilikuwa linasaidia kazi ndogo ndogo zinazohusiana na kumhudumia Lissu lakini leo dereva ametakiwa kulirudisha nchini haraka.

Tangu Lissu apigwe risasi kumekuwapo na mizengwe mingi iliyolenga kukwamisha matibabu yake ikiwamo Bunge kukataa kumgharamia matibabu, kuchelewesha Sh. milioni 41 zilizochangwa na wabunge kwa ajili ya kumsaidia Lissu.

Kauli nyingine iliyozua utata ni pale serikali iliposema tangu ya kwanza kwamba Lissu kama anataka agharamiwe matibabu ni lazima aende kutibiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na siyo vinginevyo.

Related Articles

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!