Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Somalia yaandaa mfumo wa ‘kura moja mtu mmoja’ 2021
Kimataifa

Somalia yaandaa mfumo wa ‘kura moja mtu mmoja’ 2021

Spread the love

WATAALAMU wa masuala ya uchaguzi kutoka nchi za Kiarabu na barani Afrika wamemaliza mkutano jijini Nairobi uliolenga kuipatia Somalia mfumo bora wa uchaguzi utakaohusisha utaratibu wa ‘kura moja mtu mmoja, anaandika Victoria Chance.

Somalia, nchi iliyoathirika kwa kiwango kikubwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya miongo miwili, inatarajiwa kufanya uchaguzi huru mwaka 2021, utakaokuwa wa kwanza tangu nchi hiyo ilipoingia kwenye ghasia mpya mwaka 1991 ambazo ziliikosesha serikali rasmi.

Tangu hapo nchi hii ya pembe ya Afrika haikupata kuendesha uchaguzi kutokana na kuendelea na vita vilivyohusisha makundi mbalimbali ya koo yaliyokuwa yakipigania madaraka. Tatizo kubwa la mgogoro huo ni makundi hayo kuamini katika makabila yao. Maelfu ya raia wameuawa na wengine wengi kukimbia nchi.

Ilipofika mwaka 2004 utulivu ulirejea baada ya maridhiano yaliyosaidiwa na Umoja wa Mataifa hivyo kuundwa serikali ya mpito. Pia kukaundwa bunge na serikali ikaridhiwa kuwa na makao makuu nchini Kenya. Rais aliyeongoza serikali hiyo alichaguliwa kupitia bunge hilo.

Serikali hiyo imebadilika mara tatu pasina Wasomali kupewa fursa ya kuchagua viongozi wawatakao kwa njia ya kura.

Hatimaye, mwaka jana wanasiasa wa Somalia walikubaliana kumaliza mfumo wa kuendesha nchi kwa misingi ya ukabila. Sasa wameazimia kupata mfumo wa kura moja kwa mtu mmoja.

“Mkutano huu ni hatua muhimu ya kushauri tume nyingine za uchaguzi kwa uzoefu wa kwamba mfumo wa ‘kura moja kwa mtu mmoja’ ni muhimu kwa maendeleo. Ni hatua kubwa kuelekea kwenye mfumo wa vyama vingi,” alisema mshauri wa Tume ya Uchaguzi ya Somalia, Genald Mitchell.

Pia Idris Aminu Kasimu anayefanya kazi na Tume ya Uchaguzi ya Nigeria anasema “kama hakutakuwa na demokrasia ndani ya vyama vya siasa itakuwa ni tatizo katika demokrasia ya nchi yenyewe.”

“Upo umuhimu wa demokrasia kuanzia kwenye vyama vinavyotaka kushiriki uchaguzi. Wanaotaka kugombea katika uchaguzi wan chi ni muhimu wapatikane kwa njia ya kidemokrasia maana watachaguliwa na watu wengi kwasababu uaminifu wa uchaguzi huanzia kwenye uaminifu wa chama na jinsi wagombea wanavyopatikana,” alisema Idris.

Serikali ya Somalia kwa msaada wa majeshi ya Umoja wa Afrika (AU), imedhibiti tena mamlaka kutoka kundi la wanamgambo wa Al-Shabaab, lakini bado wanamgambo hao wanaendelea kufanya mashambulizi.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Somalia, Halima Ismail Ibrahim, anasema “najua Wasomali wengi wanauliza ni vipi watapata uongozi kabla ya kuwapo mfumo wa kura moja mtu mmoja… (tume) tunaamini tukijitahidi tutafikia hatua ya kumpa fursa kila mwananchi kupiga kura yake siku ya uchaguzi.”

“Ni kazi inayopaswa kufanywa mapema iwezekanavyo, na ndio lengo la mkutano huu,” alieleza mbele ya wajumbe wa mkutano huo.

Mpango wa kuipatia Somalia mfumo wa uchaguzi wa ‘kura moja mtu mmoja’ ni utekelezaji wa ahadi ambayo Rais Hassan Sheikh Mohamud alitakiwa kuitimiza kuchagua mfumo ulio bora wa kuendesha uchaguzi mkuu. Alipewa agizo hilo kupitia azimio la Jukwaa la Taifa la Ushauri baada ya yeye rais kutamka kuwa serikali yake isingeweza kutekeleza ahadi ya mwaka 2012 iliyolenga kuiondoa nchi hiyo kutumia mfumo wa uchaguzi uliozingatia mamlaka za koo.

Uchaguzi huo ulihusisha watu milioni 4.5 waliogawiwa kikoo (koo nne kuu pamoja na muungano wa koo nyinginezo ndogo), na ushiriki wa taasisi za kidola pamoja na bunge la Senate. Asilimia 30 ya viti vya bunge la Somalia, vimetengwa kwa ajili ya wanawake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaKimataifa

Faye aahidi kuongoza kwa unyenyekevu, wagombea wenzie wakubali yaishe

Spread the loveMgombea wa upinzani Senegal, Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuwa rais...

Habari MchanganyikoKimataifa

Wanafunzi 130 waliokuwa wametekwa nyara waokolewa

Spread the loveZaidi ya wanafunzi 130 wa shule ya msingi LEA na...

Habari MchanganyikoKimataifa

Mgombea upinzani aongoza uchaguzi wa Rais Senegal

Spread the loveMgombea wa upinzani nchini Senegal, Bassirou Diomaye Faye ameonekana kuongoza...

error: Content is protected !!