Sita wakutwa na Corona EPL, Watford wagomea mazoezi

WACHEZAJI wa klabu ya Watford England wamegoma kuanza mazoezi siku ya jana kutokana na maofisa wao wawili na mchezaji mmoja kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona hali iliyopelekea kutengeneza hofu kati yao wakati wa kujiandaa na michezo ya Ligi Kuu nchini humo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mgomo huo ambao uliongozwa na nahodha wa kikosi hicho, Troy Deneey ambaye ameripotiwa kuwa hatoweza kufika kwenye viwanja vya mazoezi vya klabu hiyo kutokana na kuwepo kwa baadhi yao kuwa na maambukizi jambo ambalo limeonekana kuungwa mkono na baadhi ya wachezaji ndani ya timu hiyo.

Siku ya Jumapili wachezaji na maofisa 748 kutoka klabu mbalimbali za Ligi Kuu nchini humo walichukuliwa vipimo na sita kati yao walikutwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

Sita hao ambao wamekutwa na mambukizi ya Corona watajitenga kwa siku saba kama taratibu za nchi hiyo zilivyo kabla ya kupimwa kwa mara nyingine.

Ligi hiyo ambayo ilisamama mwezi Machi inatarajia kurudi mwezi wa sita kumalizia michezo iliyosalia huku klabu nyigi zikionekana kuanza mazoezi kwa kuchukua tahadhali zote na michezo hiyo itachezwa bila ya mashabiki.

WACHEZAJI wa klabu ya Watford England wamegoma kuanza mazoezi siku ya jana kutokana na maofisa wao wawili na mchezaji mmoja kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona hali iliyopelekea kutengeneza hofu kati yao wakati wa kujiandaa na michezo ya Ligi Kuu nchini humo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea). Mgomo huo ambao uliongozwa na nahodha wa kikosi hicho, Troy Deneey ambaye ameripotiwa kuwa hatoweza kufika kwenye viwanja vya mazoezi vya klabu hiyo kutokana na kuwepo kwa baadhi yao kuwa na maambukizi jambo ambalo limeonekana kuungwa mkono na baadhi ya wachezaji ndani ya timu hiyo. Siku ya Jumapili wachezaji…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Kelvin Mwaipungu

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram