April 11, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Simba yatambulisha beki, mshambuliaji

Joash Onyango

Spread the love

MABINGWA wa Ligi Kuu ya soka Vodacom Tanzania Bara (VPL) 2019/20 timu ya Simba, imewatambulisha wachezaji wawili mshambuliaji na beki. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Simba ambayo imetwaa taji la ligi kuu mara tatu mfululizo imesema, kuanzia leo Ijumaa tarehe 14 Agosti 2020 itakuwa inatambulisha wachezaji wapya wawili kila siku saa 8 mchana na 11 jioni.

Mchezaji wa kwanza kutambulishwa ni mshambuliaji Charles Ilamfia kutoka KMC FC ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Katika ukurasa wa Twitter, Simba imeweka picha ya Ilamafia akiwa na Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola na kuandika “kocha wetu alipomuona uwanjani kwa mara ya kwanza Charles Ilamfia akawaambia uongozi msajilini huyu kijana.”

“Miguu yake itatupa kitu Msimbazi. Ni tumaini la baadae katika soka la nchi hii hususani upande wa washambuliaji. Tumemsajili mshambuliaji toka KMC.”

Kisha saa 11 jioni kama ilivyoahidi, Simba iliyomaliza msimu ikiwa imetwaa mataji matatu Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na Kombe la FA UP, imemtambulisha beki wa Kimataifa wa Kenya, Joash Onyango akitokea timu ya Gor Mahia.

“Tumeweka malengo makubwa msimu huu ya kufika mbali kwenye ligi ya Mabingwa Afrika na mashindano ya nyumbani hivyo lazima pia klabu isajili mabeki na wachezaji wenye uzoefu mkubwa katika mechi kubwa kubwa. Beki wa kimataifa wa Kenya, Joash Onyango ametua Msimbazi,” wameandika Simba na kuweka picha ya Onyango akiwa na Matola

Onyango anaungana na wachezaji wenzake wa zamani wa Gor Mahia, Francis Kahata na Meddie Kagere.

Simba itaiwakilisha nchi katika michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika.

error: Content is protected !!