Simba yapigwa tena, Azam hoi  

Spread the love

MABIGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba wamekubali kipigo cha pili mfululizo kutoka kwa Ruvu Shooting cha 1-0. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Ruvu wameibuka na ushindi huo katika mchezo uliochezwa leo Jumatatu Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na kuwafanya kufikisha pointi 12 huku Simba ikisalia na pointi zake 13.

Kipigo hicho ni cha pili baada ya kile ilichokitapa wiki iliyopita Uwanja wa Nelson Mandela, Rukwa kutoka kwa Tanzania Prinsos.

Simba itabidi ijilaumu baada ya Nahodha wake, John Bocco kukosa mkwaju wa peneti dakika ya 80.

Peneti hiyo ilipatikana baada ya Shaban Msala kumchezea faulo ndani ya 12 mchezaji wa Simba, Bernard Morrison.

Katika mchezo mwingine uliochezwa Uwanja wa Jamhuri Morogoro, imeshuhudia Azam FC wakikubali kipigo cha kwanza tangu kuanza kwa ligi hiyo kutoka kwa Mtibwa Sugar.

Mtibwa imewafanya kufikisha pointi 11 huku Azam wakibaki na alama zao 21 kwenye michezo nane iliyocheza.

Boniface Mkwasa, Kocha wa Ruvu Shooting

Baada ya mchezo huo, nahodha wa Simba, Jonas Mkude amesema, “Tunamshukuru Mungu kwa matokeo haya, ujue mchezo wa mpira ni hivyo.”

“Tumepoteza mchezo sasa tunaangalia mchezo ujao. Ni wakati mgumu sana kwa mashabiki wetu hasa kwa hiki kinachotokea,” amesema.

Fully Maganga aliyefunga bao hilo la Simba amesema, “mimi nishawazoea Simba na kila anayekuja mbele naifunga.”

MABIGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba wamekubali kipigo cha pili mfululizo kutoka kwa Ruvu Shooting cha 1-0. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea). Ruvu wameibuka na ushindi huo katika mchezo uliochezwa leo Jumatatu Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na kuwafanya kufikisha pointi 12 huku Simba ikisalia na pointi zake 13. Kipigo hicho ni cha pili baada ya kile ilichokitapa wiki iliyopita Uwanja wa Nelson Mandela, Rukwa kutoka kwa Tanzania Prinsos. Simba itabidi ijilaumu baada ya Nahodha wake, John Bocco kukosa mkwaju wa peneti dakika ya 80. Peneti hiyo ilipatikana baada ya Shaban Msala kumchezea…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!