Simba yaonyesha umwamba kuelekea Ligi Kuu

Spread the love

KLABU ya Simba leo imeibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Transit Camp kwenye mchezo wa kujipima nguvu kuelekea kuendelea na michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayotarajia kuanza juni 13, 2020. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam…(endelea).

Katika mchezo huo magoli ya Simba yalifungwa na Deo Kanda (3), Gerson Fraga (15), Tairone Santos (17) na bao la mwisho lilifungwa na mshambuliaji wao kinara Meddie Kagere (46), huku upande wa Transit Camp mabao yao yalifungwa na Hamadi Habibu (45+1) na Nisile Kisimba (64).

Baada ya mchezo huo Simba inatarajia kushuka dimbani siku ya Jumapili kuwakabili Ruvu Shooting, kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam katika muendelezo wa mchezo wa Ligi Kuu.

Simba mpaka sasa ndio vinara kwenye msimamo wa Ligi hiyo baada ya kujikusanyia alama 72, toka Ligi hiyo ilivyosimama Machi mwaka huu kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona (Covid-19).

KLABU ya Simba leo imeibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Transit Camp kwenye mchezo wa kujipima nguvu kuelekea kuendelea na michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayotarajia kuanza juni 13, 2020. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam…(endelea). Katika mchezo huo magoli ya Simba yalifungwa na Deo Kanda (3), Gerson Fraga (15), Tairone Santos (17) na bao la mwisho lilifungwa na mshambuliaji wao kinara Meddie Kagere (46), huku upande wa Transit Camp mabao yao yalifungwa na Hamadi Habibu (45+1) na Nisile Kisimba (64). Baada ya mchezo huo Simba inatarajia kushuka dimbani siku ya Jumapili kuwakabili Ruvu Shooting, kwenye Uwanja…

Review Overview

User Rating: 2.35 ( 1 votes)

About Kelvin Mwaipungu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!