January 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Simba yaipiga Plateau 1-0, yaisubiri Dar

Spread the love

TIMU ya Simba ya Dar es Salaam nchini Tanzania, imeanza vyema michuano ya Klabu Bingwa Afrika kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Plateau United ya Nigeria. Anaripoti Kelvin Mwaipunga, Dar es Salaam …(endelea).

Mchezo huo umechezwa leo Jumapili tarehe 29 Novemba 2020 Uwanja wa New Jos nchini Nigeria na mechi ya marudiano itachezwa 5 Desemba 2020 Uwanja wa Benjamin, Dar es Salaam nchini Tanzania.

Goli pekee la Simba limefungwa Clatous Chama dakika ya 53.

Katika mchezo wa marudiano, Simba itahitaji sare ya aina yoyote au ushindi ili kuwawezesha kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

error: Content is protected !!