Simba yaanza kubeba makombe

Spread the love

TIMU ya Simba imeanza vyema safari ya msimu wa ligi 2020/21 kwa kutwaa Ngao ya Jamii. Anaripoti Kelvin Mwapungu…(endelea)

Simba ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2019/20 wametwaa Ngao hiyo leo Jumapili tarehe 30 Agosti 2020 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kwa kuwafunga Namungo FC 2-0.

Mabao hayo yamefungwa na Nahodha John Bocco na Bernad Morrison.

Bocco alifunga bao hilo dakika ya saba ya mchezo kwa mkwaju wa penati baada ya Morrison kuangushwa ndani ya eneo la hatari.

Bao hilo lilidumu hadi dakika 45 za mapumziko huku Simba ikiwa imetawala mchezo huo kwa asilimia 62 dhidi ya 38 za Namungo FC.

Dakika ya 60, Morrison aliiandikia Simba bao la pili akipokea pasi safi kutoka kwa Clatous Chama kisha kuachia mkwaju uliokwenda moja kwa moja wavuni.

Hadi dakika 90 zimamalizika, Simba walikuwa mbele kwa ushindi huo na kuwafanya kutwaa Ngao hiyo mara tatu mfululizo kama ilivyokuwa kwa kombe la Ligi Kuu.

TIMU ya Simba imeanza vyema safari ya msimu wa ligi 2020/21 kwa kutwaa Ngao ya Jamii. Anaripoti Kelvin Mwapungu…(endelea) Simba ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2019/20 wametwaa Ngao hiyo leo Jumapili tarehe 30 Agosti 2020 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kwa kuwafunga Namungo FC 2-0. Mabao hayo yamefungwa na Nahodha John Bocco na Bernad Morrison. Bocco alifunga bao hilo dakika ya saba ya mchezo kwa mkwaju wa penati baada ya Morrison kuangushwa ndani ya eneo la hatari. Bao hilo lilidumu hadi dakika 45 za mapumziko huku Simba ikiwa imetawala mchezo huo kwa…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Kelvin Mwaipungu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!