Simba mguu sawa kuivaa Namungo FC

Spread the love

KLABU ya Simba imecheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya KMC na Transit Camp kujiweka sawa kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Namungo FC, unaotarajiwa kuchezwa 30 Agosti, 2020 mkoani Arusha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Michezo hiyo ilipigwa kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam ambapo mchezo wa kwanza Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya KMC, na mchezo wa pili klabu hiyo ilifanikiwa kupata ushindi mbele ya Transit Camp kwa mabao 5-2.

Kwenye mchezo dhidi ya KMC mabao ya Simba yalifungwa na Clotus Chama 28, Ibrahim Ajibu 33 na Mzamiru Yassin 57, huku kwenye mchezo wa Transit Camp mabao ya samba yalipachikwa na Kipenye 4, 24, Charles Ilanfya 19, Meddy Kagere 42 na Gardiel Michael kwenye dakika ya 79.

Simba

Kufuatia mchezo huo Simba itakuwa inajiandaa na safari ya kuelekea mkoani Arusha kwenye mchezo huo ambao unatarajia kuchezwa majira ya saa 9:30, ambao utakuwa unaashilia kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2020/21.

KLABU ya Simba imecheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya KMC na Transit Camp kujiweka sawa kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Namungo FC, unaotarajiwa kuchezwa 30 Agosti, 2020 mkoani Arusha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea). Michezo hiyo ilipigwa kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam ambapo mchezo wa kwanza Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya KMC, na mchezo wa pili klabu hiyo ilifanikiwa kupata ushindi mbele ya Transit Camp kwa mabao 5-2. Kwenye mchezo dhidi ya KMC mabao ya Simba yalifungwa na Clotus Chama…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Kelvin Mwaipungu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!