January 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Simba kuivaa Kagera, Yanga yarejea Dar

Spread the love

KLABU ya Simba leo Jumatano tarehe 4 Novemba 2020 itashuka dimbani kwenye mchezo wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara 2020/21 dhidi ya Kagera Sugar katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Anaripoti Kelvin Mwaipungu… (endelea).

Wakati Simba ikishuka dimbani, wapinzani wao watakao kutana kwenye mchezo ujao Yanga imerejea Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya maandalizi kuelekea mchezo huo utakaopigwa Jumamosi 7 Novemba 2020, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Mchezo huo wa Simba leo dhidi ya Kagera Sugar utachezwa saa 10 jioni huku ukiwa kama sehemu ya mandalizi kuelekea mchezo wao dhidi ya Yanga.

Yanga imerejea jana usiku Jumanne kutoka jijini Mwanza ambapo walikuwa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Gwambina FC na kuambulia pointi moja mara baada ya kwenda sare ya bila kufungana.

Mashabiki wa timu ya Yanga

Matokeo hayo ya mchezo wa jana wa Yanga, yataichagiza Simba kuingia kwa nguvu zote kwenye mchezo wao dhidi ya Kagera huku wakihitaji pointi tatu ambazo zitawasaidia kupunguza uwiano wa pointi sita ambazo walizokuwa wameachwa awali.

Mpaka sasa, Yanga imecheza jumla ya michezo tisa huku ikiwa na pointi 23 huku ikiicha Simba kwa tofauti ya pointi saba ambayo imecheza michezo nane na kujikusanyia jumla ya pointi 16.

Mchezo huu wa Simba dhidi ya Kagera Sugar itatoa taswira kuelekea mchezo ujapo wa watani wa jadi ambao klabu ya Yanga itakuwa mwenyeji wa mchezo huo.

Watani hao wa jadi watakutana siku ya jumamosi 7 Novemba 2020 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam majira ya saa 11 jioni katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 200/21.

error: Content is protected !!