Sikuhonga kupata urais – JPM

Spread the love

DAKTARI John Pombe Magufuli, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema, hakuhonga kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anaripoti Brightness Boaz, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza kwenye mkutano wake wa kampeni alioufanya leo Jumatatu tarehe 12 Oktoba 2020 katika Jimbo la Segerea, Ilala jijini Dar es Salaam amesema, hakutarajia kuwa rais na kazi hiyo amepewa na Mungu.

“… sikujua mimi kwamba siku moja nitakuwa rais na wala sikutegemea kuwa rais, baada ya Kikwete (Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu), aliyefuata ni Magufuli.”

“Nimefanya kazi katika kipindi changu cha miaka mitano na kwa sababu urais ule niliupata bila kutumwa na mtu, bila kuhonga, mimi nilijua kuwa Mungu ndiye aliyenipa hii kazi kama sadaka ya kuwafanyia kazi Watanzania…,” amesema Dk. Magufuli.

Amesema, wakati anaanza kuongoza Taifa hili tarehe 5 Novemba 2015, alikumbana na changamoto kubwa ya kwanza kuhusu amani na usalama kwa wananchi.

Na kwamba, hakuwa tayari kuona hali hiyo ikiendelea kuimarika sehemu mbalimbali nchini, hivyo alipambana na kurejesha usalama kwenye maeneo hayo.

“Tulipoingia, changamoto zilikuwepo, palikuwa na maeneo ambayo hanaya amani na utulivu. Ukienda Kibiti (Pwani) watu wameuawa mpaka maaskari zaidi ya 17 walipigwa risasi.”

“Hiyo ilikuwa chalenji yangu ya kwanza. Ukienda Kigoma, ukienda Bukoba ulikuwa huwezi kwenda kwa gari mpaka usindikizwe na polisi, watu walikuwa wanaiba mchana,” amesema Magufuli na kuongeza:

“Pale Ubungo paliwahi mtu kuvamia benki, mchana watu wanapiga bunduki. Nikasema ndani ya utawala wangu, hili lazima nilikomeshe.”

Amesema, katika utafiti uliofanya na benki ya dunia ulisema, jiji la Dar es salaam lilikuwa linapoteza bilioni nne kwa sababu ya foleni na ndio maana aliamua kufanya mkakati wa kulitatua ikiwemo kufanya ujenzi wa barabara za juu kama Ulaya na daraja la Kwa Mfugale lililopo Tazara.

Na kwamba, alipoingia madarakani mwaka 2015 alikuwa na dhamira ya kuibadili Dar es Salaam lakini wakazi wa jiji hilo walichagua wabunge na madiwani wengi wa upande mwingine hivyo kumpunguza kasi.

Dk. Magufuli amewashukuru viongozi wote wa dini kwa kuwa mstari wa mbele kuliombea Taifa.

DAKTARI John Pombe Magufuli, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema, hakuhonga kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anaripoti Brightness Boaz, Dar es Salaam … (endelea). Akizungumza kwenye mkutano wake wa kampeni alioufanya leo Jumatatu tarehe 12 Oktoba 2020 katika Jimbo la Segerea, Ilala jijini Dar es Salaam amesema, hakutarajia kuwa rais na kazi hiyo amepewa na Mungu. “… sikujua mimi kwamba siku moja nitakuwa rais na wala sikutegemea kuwa rais, baada ya Kikwete (Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu), aliyefuata ni Magufuli.” “Nimefanya kazi katika kipindi changu cha miaka mitano na kwa sababu urais ule niliupata…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!