Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Siku saba ngumu kwa Membe, Kinana, Mzee Makamba ndani ya CCM
Habari za SiasaTangulizi

Siku saba ngumu kwa Membe, Kinana, Mzee Makamba ndani ya CCM

Spread the love

KAMATI Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM),  imetoa siku saba kwa Kamati Ndogo ya Udhibiti na Nidhamu, kukamilisha taarifa ya mahojiano ya Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje Mstaafu na Makatibu Wakuu Wastaafu wa chama hicho, Mzee Yusuph Makamba na Abdulrahman Kinana. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi (CCM) , imesema Kamati Kuu iliyoketi leo tarehe 12 Februari 2020 jijini Dar es Salaam, chini ya Rais John Magufuli, imeitaka kamati hiyo kuwasilisha taarifa hiyo kwenye vikao husika.

Aidha, taarifa ya Polepole inaeleza kwamba, Kamati Kuu ya CCM imepokea taarifa ya awali kutoka kwa kamati hiyo ndogo ya udhibiti na nidhamu.

“Kamati Kuu imepokea taarifa ya awali kutoka kwa Kamati ya Usalama na Maadili juu ya utekelezaji wa azimio la Halmashauri Kuu ya Taifa katika kikao chake cha mwezi Desemba jijini Mwanza kuhusu kuwaita na kuwahoji wanachama watatu, Mzee Makamba, Kinana na Membe ambao wote wameshafika mbele ya Kamati Mdogo ya Udhibiti na Nidhamu inayoongozwa na Mzee Phillip Mangula,” inaeleza taarifa ya Polepole na kuongeza:

“Kamati Kuu imetoa siku saba kwa Kamati Ndogo ya Udhibiti na Nidhamu, kukamilisha taarifa inayowahusu wanachama hawa watatu na kuwasilisha katika vikao husika.”

Agizo hilo la Kamati Kuu ya CCM, limetolewa siku kadhaa baada ya wanachama hao wa CCM kuhojiwa na kamati hiyo katika nyakati tofauti, ambapo Membe alihojiwa jijini Dodoma wakati Mzee Makamba na Kinana wakihojiwa jijini Dar es Salaam.

Wanachama hao wa CCM wanatuhuma kwa kukiuka maadili ya chama hicho kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo madai ya kutoa kauli zinazodhalilisha viongozi wa serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!