Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Siku 100 za Chadema Ikulu
Habari za Siasa

Siku 100 za Chadema Ikulu

John Mrema, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje Chadema
Spread the love

NDANI ya siku 100 za utawala mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), endapo kitapata ridhaa ya wananchi, zitakuwa za kimapinduzi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ufafanuzi wa namna Chadema itakavyotumia siku 100 za kwanza umetolewa na John Mrema, Mkurugenzi wa Itifaki Chadema leo tarehe 4 Agosti 2020, wakati akisoma muhtasari wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, 2020 ya chama hicho, kwenye Mkutano Mkuu unaondelea Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

Mrema amesema, suala la kwanza ambalo Chadema itafanya kama itafanikiwa kushinda katika uchaguzi huo, itapeleka bungeni Muswada wa Sheria ya Maridhiano sambamba na kuanzisha Tume ya Maridhiano.

“Siku 100 tangu Rais wa Chadema atakapoapishwa, serikali  itapeleka bungeni muswada wa sheria ya maridhiano, itaanzisha tume ya maridhiano kwa ajili ya kuondoa hofu ya uwezekano wa vitendo vya kikasi, bila ubaguzi wa kiitikadi, rangi kwa lengo la kuunganisha Taifa ambalo sasa limepa suka pasuka,” amesema Mrema.

Mrema amesema, suala la pili ambalo Serikali ya Chadema itafanya ni kupeleka bungeni muswada wa Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi juu ya utoaji elimu bure kuanzia shule ya awali hadi sekondari.

Mkurugenzi huyo wa Itifaki Chadema amesema, serikali ya chama hicho itapunguza kiwango cha marejesho ya mikopo kwa wanufaika wa mkopo wa elimu ya juu, kutoka asilimia 15 wanayotozwa sasa hadi kufikia asilimia tatu.

“Wanafunzi wa elimu ya juu na wanufaika, Serikali ya Chadema itapunguza kiwango cha marejesho ya mikopo hadi kufikia asilimia 3, sio 15 ya mshahara wa mnufaika na kutanua wigo wa muda wa kurejesha wa miaka 25 tangu wanapoipata ajira,” amesema Mrema.

Sambamba na hilo, Mrema amesema Serikali ya Chadema itafuta faini ya ucheleweshaji kurejesha fedha za mikopo.

“Serikali ya Chadema  itashirikiana na sekta binafsi kuweka utaratibu kutoa huduma ya afya za msingi bila malipo, lengo letu ni kwamba  ugonjwa hautoi tahadhari unakuja kesho,  leo nchi yetu ugonjwa ukija kama huna pesa taslimu, huwezi kumuona tabibu.

Tutaweka utaratib uwe wa bima au nyingine mtu atibiwe kwanza akatafute pesa arudi kulipa kuliko watu wafe sababu hawana pesa,” amesema Mrema.

Mrema amesema, Serikali ya Chadema itarejesha mchakato wa upatikanaji Katiba Mpya uliosisiwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Joseph Warioba.

“Serikali ya Chadema itarejesha mchakato wa Katiba Mpya kuanzia ilipoishia rasimu ya Jaji Warioba, tunakwenda kuchukua yale maoni mliyosema wananchi, tuendelee hapo kwa ajili ya kuipatia nchi katiba mpya na hiyo tutafanya ndani ya siku 100 za kwanza,” amesema Mrema.

Sambamba na hilo, Mrema amesema Serikali ya Chadema itaifufua Tume ya Pamoja ya Fedha za Muungano.

Mrema amesema “Serikali ya Chadema itapeleka miswada ya sheria bungeni kwa dhumuni la kufuta sheria kandamizi zinazokiuka haki za binadamu, hilo tunafanya katika Bunge la kwanza. “

“Serikali ya Chadema itaanzisha utaratibu wa mazungumzo kati ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanmzibar kwa lengo la kufikia muafaka juu ya utafutaji na uchimbaji mafuta, gesi , usajili wa meli na uvuvi,” amesema Mrema.

Mrema amesema Chadema kikifanikiwa kuingia madarakani , Serikali yake itapeleka bungeni bajeti ya nyongeza kwa ajili ya kulipa malimbikizo ya madeni ya watumishi sambamba na kupandisha madaraja.

2 Comments

  • Mpo vizuri chadema CCM ya magufuli mpka leo imetnyima malipo ya madeni yetu Toka mwka 2013 wanaolpwa Ni wanaojulikana,hela za likizo imekua Ni Kama ofa sio haki kwa mtumishi wa umma mishahra aipndi, nashangaa kuona serikali kuweza kununua madini tanzanite ya mmsai hko Arusha, Kama Mali ipo si serikali inunue mitambo tukchmbe tuuze hela zptkane

  • Sijaona mnasema vile mtakavyokaa na vyama vingine kuondoa kero mnayopiga nayo kelele kila siku ya Tume huru ya uchaguzi 😂😂😂 Au ndio itakuwaje 🤔🤔🤔 Wana siasa wa Afrika tubedilike hatwendi mahali kokote na sera hizo. Sioni radical transformation yoyote kwenye hayo mliyozunguzia mnazunguka mbuyu. Flag bearer wenu anajua kulumbana in court na mitaani sasa ukimlinganisha na Raisi aliye madarakani sasa ni vitu tofauti kwenye kuleta maendeleo. Na watanzania mkifanya makosa mkaenda huko sijui wapi yani msahau maendeleo kwa kipindi kingine cha miaka 30 mpaka 50. Maono uelewa ujunzi na hari ya Magufuli hakuna kiongozi yoyote Tanzania ambayo unaweza kumlinganisha naye tuwe wakweli na wazalendo kwa manufaa ya taifa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!