Rais John Magufuli

Shule zote Tanzania kufunguliwa Juni 29

Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli ameagiza shule zote nchini humo zifunguliwe tarehe 29 Juni 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea),

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo Jumanne tarehe 16 Juni 2020 wakati akihutubia Bunge jijini Dodoma.

Amesema, hali ya maambukizi ya ugonjwa wa vurusi vya corona (Covid-19) yamepungua.

Pia, Rais Magufuli ameagiza shunguli zingine nazo zirejee, “maisha ni lazima yarudi kama yalivyokuwa zamani.”

Shule hizo zilifungwa tangu tarehe 17 Machi 2020 ili kuepuka maambukizo ya corona.

Jana Jumatatu tarehe 15 Juni 2020, Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa alihitimisha mkutano wa 19 wa Bunge hilo la 11, alisema maambukizi hayo yamepunguza na wagonjwa waliopo ni 66 pekee.

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli ameagiza shule zote nchini humo zifunguliwe tarehe 29 Juni 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea), Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo Jumanne tarehe 16 Juni 2020 wakati akihutubia Bunge jijini Dodoma. Amesema, hali ya maambukizi ya ugonjwa wa vurusi vya corona (Covid-19) yamepungua. Pia, Rais Magufuli ameagiza shunguli zingine nazo zirejee, “maisha ni lazima yarudi kama yalivyokuwa zamani.” Shule hizo zilifungwa tangu tarehe 17 Machi 2020 ili kuepuka maambukizo ya corona. Jana Jumatatu tarehe 15 Juni 2020, Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa alihitimisha mkutano wa 19 wa Bunge hilo la 11, alisema…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!