John Shibuda, aliyekuwa mbunge wa Maswa Magharibi

Shibuda: Msindai, Mpendazowe wanafiki

Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

HATUA ya Fredy Mpendazowe na Mgana Msindai kurudi Chama Cha Mapinduzi (CCM), inatokana na kuhangaikia maslahi binafsi, anaandika Dany Tibason.

Msindai, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida alijiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kabla ya Uchaguzi Mkuu mwaka jana kwa madai, ndani ya CCM hakuna demokrasia.

John Shibuda, Katibu Mkuu wa Chama cha ADA TADEA amesema, wakongwe hao katika siasa waliondoka CCM kwa madai ya kukerwa na chama hicho lakini cha kushangaza wamerejea kwa mbwembwe.

Shibuda amesema kwamba, wanasiasa hao ni wanafiki ndani ya siasa na kuwa “mnafiki hafi hadi ameumbuka.” Amedai hatua ya kurejea CCM imewaumbua.

“Waliishambulia CCM wakiwa kwenye majukwaa ya Chadema, leo wamerejea kule walikokuwa wakishambulia,” amesema Shibuda.

Amesema, Mpendazowe na Msindai wamekuwa wakiuaminisha umma kwamba CCM ni chama cha hovyo “iweje leo warejee kule kule kwa hovyo?

“Watu wazima kama hao ni wanafiki ndani ya siasa na wamekula matapishi yao. Hawawezi kuaminika tena katika jamii na katika ulingo wa siasa kwa kuwa, ni wanasiasa maslahi.

“Siyo wanasiasa bali wamevaa vazi la siasa huku uhalisia ukiwa ni wanasiasa maslahi. Hakukuwa na maana kutumia majukwaa kuitukana CCM na baadaye kurudi.

“Walipotoka CCM kwenda Chadema walitumia majukwaa kuishambulia CCM na sasa wamerudi CCM kwa kuishambulia Chadema.”

Shibuda amesema, umri wa wanasiasa hao ulitakiwa kutumiwa kuwajenga vijana kifikra juu ya kuwepo kwa siasa safi ambazo ni za ukombozi.

“Kwa umri wa Msindai na Mpendazowe walitakiwa kuwa shamba darasa na urithi wa mawazo kwa vijana chipukizi wa kisiasa.

“Tujikumbushe jinsi Mpendazoe alivyoweza kutunga kitabu ambacho kiliweza kuelezea mambo mengi, leo ni aibu kwa msomi huyo kuonesha udhaifu wa kisiasa na kujidhalilisha,” amesema Shibuda.

Pia ameishangaa CCM kwa kuwapokea wanasiasa wachafu na ambao wamekuwa wakikisema chama hicho vibaya hadharani.

“Kauli ya Rais John Magufuli kudai anataka usafi ndani ya chama ni unafiki, sidahi kama kuna kanisa ambalo linaweza kumpokea muumini ambaye aliyemkataa Yesu au msikiti ambao unaweza kumkaribisha muumini ambaye alimkataa Mtume.

“Je, muumini wa Dini ya Kiislamu anaweza kuitukana Qur’an na baadaye akaanza kuisifia? hilo jambo haliwezekani.”

Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn
HATUA ya Fredy Mpendazowe na Mgana Msindai kurudi Chama Cha Mapinduzi (CCM), inatokana na kuhangaikia maslahi binafsi, anaandika Dany Tibason. Msindai, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida alijiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kabla ya Uchaguzi Mkuu mwaka jana kwa madai, ndani ya CCM hakuna demokrasia. John Shibuda, Katibu Mkuu wa Chama cha ADA TADEA amesema, wakongwe hao katika siasa waliondoka CCM kwa madai ya kukerwa na chama hicho lakini cha kushangaza wamerejea kwa mbwembwe. Shibuda amesema kwamba, wanasiasa hao ni wanafiki ndani ya siasa na kuwa “mnafiki hafi hadi ameumbuka.” Amedai hatua ya kurejea CCM imewaumbua.…

Review Overview

User Rating: 3.45 ( 2 votes)
0

About Dany Tibason

  • TWAHA MRUMA

    Siasa na unafiki vinakwenda pamoja. Wa-TZ hawajasahau jinsi chama kimoja kilivyozunguka nchi nzima kuwaaminisha wa-TZ kwamba mtu fulani ni fisadi mkubwa. Lkn chama hicho hicho kikamsafisha chini ya saa moja na kumtangaza kuwa ni mgombea wao wa urais. Cha kusikitisha ni kwamba walimtosa yule jamaa wa Karatu aliyekijenga chama hicho na sasa hawataki hata kumsikia. Kila mmoja apime kwa wakati wake, ni chama kipi kimejaa unafiki na wanafiki.

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube