Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Sherehe za Muungazo zapigwa ‘stop’

Spread the love

SERIKALI imesitisha sherehe za kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Hayo amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akizungumza ofisini kwake jijini Dodoma leo tarehe 25 Aprili 2019.

Waziri Majaliwa amesema kiasi cha fedha Sh. 988.9 milioni ambazo zilitengwa kwa ajili ya sherehe hizo ambazo zilitarajiwa kufanyika tarehe 26 Aprili 2019, zimeokolewa na kwamba zitapangiwa matumizi mengine.

Waziri Majaliwa amesema tarehe 26 Aprili 2019 itakuwa ni siku ya mapumziko kwa ajili ya kuadhimisha muungano huo, na hakutakuwa na shamrashamra za aina yoyote ile.

SERIKALI imesitisha sherehe za kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Anaripoti Regina Mkonde ... (endelea). Hayo amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akizungumza ofisini kwake jijini Dodoma leo tarehe 25 Aprili 2019. Waziri Majaliwa amesema kiasi cha fedha Sh. 988.9 milioni ambazo zilitengwa kwa ajili ya sherehe hizo ambazo zilitarajiwa kufanyika tarehe 26 Aprili 2019, zimeokolewa na kwamba zitapangiwa matumizi mengine. Waziri Majaliwa amesema tarehe 26 Aprili 2019 itakuwa ni siku ya mapumziko kwa ajili ya kuadhimisha muungano huo, na hakutakuwa na shamrashamra za aina yoyote ile.

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Regina Mkonde

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!