Sheikh Ponda akiwa ndani ya kituo cha televisheni cha Horizon cha nchini Kenya
Sheikh Ponda akiwa ndani ya kituo cha televisheni cha Horizon cha nchini Kenya

Sheikh Ponda: Nimemwona Lissu, nimeumia

KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, Sheikh Issa Ponda ameueleza mtandao huu kwamba, amefanya mazungumzo na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanzania, Tundu Lissu anayendelea na matibabu jijini Nairobi nchini Kenya, anaandika Faki Sosi.

Kiongozi huyo wa dini ametoa kauli hiyo leo baada ya kuulizwa na mtandao huu kuhusu safari na malengo yake nchini Kenya ambapo amesema, ilihusu masuala ya kijamii.

“Nikiwa kwenye safari yangu ya masuala ya kijamii nchini Kenya, nimeonana na Mheshimiwa Lissu hospitalini alikolazwa, nilienda kumjulia hali na kufanya naye mazungumzo.”

Sheikh Ponda amesema “Kwa kweli tukio la Mheshimiwa Lissu linaumiza, nimefanikiwa kumwona, lakini nimepanga kuzungumza na vyombo vya habari nchini kuhusu mazungumzo yangu na Mheshimiwa Lissu kesho (Jumatano), naomba uwe na subra mpaka kesho.”

Kwa uchache Sheikh Ponda amesema, pamoja na kumtembelea Lissu, alipata fursa ya kutembelea Kituo cha Televisheni cha Horizon (HORIZON TV).

KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, Sheikh Issa Ponda ameueleza mtandao huu kwamba, amefanya mazungumzo na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanzania, Tundu Lissu anayendelea na matibabu jijini Nairobi nchini Kenya, anaandika Faki Sosi. Kiongozi huyo wa dini ametoa kauli hiyo leo baada ya kuulizwa na mtandao huu kuhusu safari na malengo yake nchini Kenya ambapo amesema, ilihusu masuala ya kijamii. “Nikiwa kwenye safari yangu ya masuala ya kijamii nchini Kenya, nimeonana na Mheshimiwa Lissu hospitalini alikolazwa, nilienda kumjulia hali na kufanya naye mazungumzo.” Sheikh Ponda amesema “Kwa kweli tukio la Mheshimiwa Lissu linaumiza, nimefanikiwa kumwona, lakini nimepanga kuzungumza…

Review Overview

User Rating: 3.15 ( 1 votes)
0

About Faki Sosi

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube