Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sheikh Ponda amfuata Lissu jukwaani
Habari za SiasaTangulizi

Sheikh Ponda amfuata Lissu jukwaani

Spread the love

SHEIKH Ponda Issa Ponda, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini, amempigia kampeni Tundu Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Kwenye kampeni zake za urais jijini Dodoma jana tarehe 17 Oktoba 2020, Sheikh Ponda alipopewa kipaza sauti, alisema “Tanzania mpya oyeee!” kauli hiyo aliyoitoa kwa kuirudia rudia mara kadhaa, iliitikiwa na wafuasi wa chama hicho “Oyeee!” Kisha akasema “rais mpya oyeee!” wakajibu “oyeeee!

Kwenye kampeni hizo Lissu amewaambia wafuasi wa chama hicho kwamba, kwa muda mrefu alimuomba Sheikh Ponda kuwa naye.

Hata hivyo, kwenye kipindi chote hicho Sheikh Ponda hakutokea, na kwamba amemshukuru kwa kukubali ombi lake la kukaa naye kwenye jukwaa hilo.

“Sheikh Ponda ni mtu wa haki, na nimefurahi sana Sheikh Ponda umekuja. Katika viongozi wengi wa kidini, Sheikh Ponda alikuja kuniona Nairobi (Kenya), aliporudi mnajua yaliyomkuta, alikamatwa.

“Kwa hiyo nimefurahi sana, Sheikh Ponda karibu sana na karibu kwenye msafara huu. Nimekuomba mara nyingi uje, nimefurahi sana umekuja, asante sana,” amesema Lissu wakati akimtambulisha kiongozi huyo wa dini.

Baada ya kauli hiyo, Sheikh Ponda aliinuka kutoka kwenye kiti alichokuwa amekaa na kumfuata Lissu, kisha alimpa mkono.

Lissu amesema, Sheikh Ponda kwa kuwa, ni miongoni mwa viongozi wa dini wanaopenda haki.

“Nilishasema hadharani siku nyingi, mimi sio muislam lakini binadamu ni binadamu…, kama sintamtetea huyu ambaye sina imani yake, siku yakinikuta mie nani atakayenisemea?” amesema Lissu.

Kwenye mkutano huo, Lissu amelalamika kutopata msaada wowote kutoka Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma “katika makao makuu ya nchi yetu, tumeachwa hivi hivi na Jeshi la Polisi la mkoa huu, tunajihangaikia wenyewe barabarani.

“Yaani IGP (Simon Sirro) kama unanisikia, huna RPC (mkuu wa jeshi la polisi wa mkoa) hapa…., inakuwaje mgombea urais yeye ndiye anayeongoza msafara kwenye malori makubwa kama haya?

“Ni utendaji gani huu? Tumesindikizwa kila mahali na polisi isipokuwa hapa Makao Makuu ya nchi,” amesema.

1 Comment

  • Kama sheikh Ponda anazungumza kwa niaba ya jumuiya ya Waislamu itakuwa ni kosa, sawa na Mufti kumpigia kampeni JPM kwa niaba ya Bakwata ni kosa

    Mwislamu ana haki ya kufuata chama chochote lakini hana haki ya kuzungumzia kwa niaba ya jumuiya ya Waislamu kwa sababu hiyo ni haki ya raia kujiamulia mwenyewe siyo kuamuliwa na Mufti au na Ponda

    hali kadhalika na mitume na wachungaji na maaskofu

    WAKUU WA DINI MSITUMIE MAJUKWAA YA KIDINI KUSHAWISHI VYAMA VYA SIASA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!