Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Shahidi ‘fundi magrili’ amng’ang’ania Mbowe, Matiko, Mdee kuhusika
Habari za SiasaTangulizi

Shahidi ‘fundi magrili’ amng’ang’ania Mbowe, Matiko, Mdee kuhusika

Wanachama wa Chadema wakiwa katika maandamano huku Polisi wakiwa tayari kuwakabili
Spread the love

LEO tarehe 14 Mei 2019, shahidi wa pili upande wa serikali kwenye kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi wa Chadema, ametoa ushahidi wake.

Jopo la mawakili wa serikali linaongozwa na Faraja Nchimbi, Wankyo Simon na Paul Kadushi. Huku upande wa utetezi ukiongozwa na Profesa Abdallah Safari, Peter Kibala na John Malya.

Shahidi wa pili ni Shabani Hassan Abdallah (19) chini ya kiapo, ametoa ushahidi wake akiongozwa na Kadushi.

Kadushi: Unaishi wapi?

Shahidi: Kinondoni Moscow.

Kudushi: Unafanya kazi gani?

Shahidi: Kazi ya welding (kuchomea) vitanda, mageti, madirisha na vitu vinavyohusiana na chuma.

Kudushi: Hii kazi unaifanyia wapi?

Shahidi: Eneo la Mkwajuni.

Kudushi: Eneo la Mkwajuni umesema lipi kati ya wapi na wapi?

Shahidi: Magomeni Moroko na Kinondoni.

Kudushi: Umefanya kazi hii tangu lini?

Shahidi: Mwaka 2017 mwishoni hadi sasa hivi.

Kudushi: Kabla ya hii kazi, ulikuwa wapi?

Shahidi: Nasoma.

Kudushi: Wapi?

Shahidi: Moshi

Kudushi: Shule gani?

Shahidi: Msasani Sekondari School.

Kudushi: Ulimaliza lini?

Shahidi: 2017

Kudushi: Level gani?

Shahidi: Kidato cha nne.

Kudushi: Ulipomaliza matokeo yalikuwaje?

Shahidi: Nilifaulu kuendelea na kidato cha tano.

Kudushi: Nini kilitokea.

Shahidi: Nilikosa fedha za kuendelea na masomo. Dada angu aliongea na mama yangu ndipo nilipotumiwa nauli na nikaja huku Dar kwa dada yangu Mariamu.

Kudushi: Ulipofika kwa dada yako Mariamu, nini kiliendelea?

Shahidi: Dada yangu na shemeji walisema nichukue ujuzi. Shemeji yangu Haju Ramadhani.

Kudushi: Baadaye ilikuwaje?

Shahidi: Siku hiyo walinipigia simu niende Mkwajuni ambapo alinikutanisha na bosi na alinitambulisha kijana wetu anataka kazi, nilianza kupiga rangi kwenye ofisi hiyo ya uchomeaji.

Kudushi: Ulipiga rangi vitu gani?

Shahidi: Vitanda, mageti na madirisha

Kudushi: Eneo unalofanyia kazi lipo eneo gani?

Shahidi: Kushoto kutoka Moroco kwenda magomeni na kulia ukitoka Magomeni kwenda Moroco ya Barabara ya Kawawa.

Kudushi: Kwa ufupi makubaliano yapoje?

Shahidi: Nalipwa kutokana na maridhio ya bosi au ije kazi ya mtu binafsi.

Kudushi: Unakumbuka nini siku ya tarehe 16 Februali 2017 asubuhi?

Shahidi: Nilikuwa nyumbani, ilipofika saa mbili nikaingia kazini.

Kudushi: Eneo hasa la kazi yako linaitwaje?

Shahidi: Meredian bet.

Kudushi: Pale unapofanyika kazi panaitwaje?

Shahidi: Seba Steel Furtniture.

Kudushi: Unaweza kutuelezea hilo eneo lipoje?

Shahidi: Unaposhuka pembeni ya kituo unakutana na fremu ya kwanza Meredian Bet, ya pili Stationary, inayofuata kuna mama anauza nguo fremu inayofuata ni ya kwetu sisi. Inayofuata kuna mdada anauza nguo za Kiislamu.

Kudushi: Umefika kazi saa 2 ulifanya nini?

Shahidi: Nimefanya kazi ya kusafisha kitanda.

Kudushi: Ulifanya kazi hii hadi muda gani?

Shahidi: Nimefanya mpaka saa nne…. baadaye ulifika muda wa kuswali.

Kudushi: Kuswali saa ngapi?

Shahidi: Saa 7.

Kudushi: Ulipomaliza kuswali.

Shahidi: Nirudi kazini.

Kudushi: Saa ngapi?

Shahidi: Niliswali saa 7 na dakika 10 na saa saba na dakika 20 ndio nilirudi kazini.

Kudushi: Nini kiliendelea baada ya hiyo saa nane?

Shahidi: Bosi alikuja, alichelewa kidogo baada ya kufika alituita mafundi wote na kupanga utaratibu wa kazi.

Kudushi: Baada ya hapo?

Shahidi: Tulichukua pesa ilikuwa majira ya saa 11 kuelekea saa 12 jioni.

Kudushi: Hiyo ilichukua kwa kazi gani?

Shahidi: Nilikwenda kununua vifaa.

Kudushi: Baada ya kuchukua fedha, nini kiliendelea?

Shahidi: Nilichukua fedha nikaenda duka la Hardware (vifaa vya ujenzi).

Kudushi: Ulienda kununua vifaa vipi?

Shahidi: Nilienda kununua mabomba kwa ajili ya miguu ya kitanda na stiki.

Kudushi: Mwenye hiyo hardware anaitwa nani?

Shahidi: Tunamuita baba mdogo au baba John.

Kudushi: Hiyo stiki kwa ajili ya nini?

Shahidi: Bomba kwa ajili ya miguu Flat Bat kwa ajili ya chaga na stili kuchomea. Tulikuwa tunafanya mahesabu kabla ya kichukua hivyo vitu.

Kudushi: Na hii hardware ya Baba John ipo eneo gani?

Shahidi: Mkwajuni pembezoni mwa Barabara ya Kawawa.

Kudushi: Mlipokuwa mnaendelea kupiga mahesabu, nini kiliendelea?

Shahidi: Kwa mbali nilisikia zogo.

Kudushi: Nini kilijili?

Shahidi: Hatukuweza kufuatilia kwasababu sauti zilikuwa mbali lakini baadaye sauti zilizidi kupanda juu.

Kudushi: Nini kiliendelea?

Shahidi: Mimi na Baba John tulisogea pembezo ya barabara na tukawaona watu wanaofika 200 katikati ya barabara.

Kudushi: Nini kiliendelea?

Shahidi: Wale walikuja kwa mbele wakitokea Moroco kuelekea Magomeni.

Kudushi: Wewe binafsi uliona nini?

Shahidi: Niliona watu wengi wameshika mawe, marungu na bendera.

Kudushi: Walikuwa katika hali gani hawa watu?

Shahidi: Walikuwa katika hali ya shari.

Kudushi: Unamaanisha nini?

Shahidi: Hali ambayo kama wanakwenda kupigana na watu.

Kudushi: Nini kiliendelea baadaye?

Shahidi: Walikuwa wakitusogelea.

Kudushi: Walikuwa wakifanya nini?

Shahidi: Walikuwa wakiimbia.

Kudushi: Wakiimba nini?

Shahidi: Hatupoi mpaka mmoja afe ‘mtatuua mtatuua’.

Kudushi: Mlibaini?

Shahidi: Tuliambizana na Baba John, tukasema watu wa Chadema wale.

Kudushi: Nini kilichokufanya ujue kuwa, hao ni watu wa Chadema?

Shahidi: Walikuwa wamevaa skafu na sare za Chadema.

Kudushi: Nini ulikiona baadaye?

Shahidi: Niliona wafuasi mbele yao viongozi wa Chadema.

Kudushi: Unaweza kuwatambua?

Shahidi: Baadhi naweza kuwatambua.

Kudushi: Kina nani?

Shahidi: Alikuwa Mbowe, Matiko, John, Halima Mdee.

Kudushi: Unawafahamu kama kina nani?

Shahidi: Viongozi wa chama cha Chadema.

Kudushi: Wale watu uliosema uliona zogo na uliona wameshika nini na wakasogea ulikuchukua muda gani hadi kuwatambua.

Shahidi: Kwasababu walikuwa wanakuja mbele, walivyokuwa wakisogea ndio tunawatambua vizuri.

Kudushi: Ili kujiridhisha ulifanyaje kujua kuwa hao ni viongozi wa Chadema.

Shahidi: Nawaonaga kwenye magazeti kwenye TV.

Kudushi: Ulikuwa ukiwaona kama kina nani?

Shahidi: Viongozi wa chama. Baada ya hapo niliona gari la askari likiwatangazia watawanyike.

Kudushi: Kina watawanyike?

Shahidi: Wale waliokuwa wameandamana.

Kudushi: Na uliona nini zaidi?

Shahidi: Walikuwa wameshika vipaza sauti na walikuwa wakikatiza kati yao.

Kudushi: Watu hao walikuwa wapi?

Shahidi: Wametanda kwenye barabara

Kudushi: Nini kiliendelea?

Shahidi: Walikatiza mbele yao na kuwatangazia.

Kudushi: Watu gani?

Shahidi: Askari

Kudushi: Nini kilitokea?

Shahidi: Baadaye walionekana kuwa, hawakukubali kushindwa waliwasogolea wale askari.

Kudushi: Baada ya hapo, nini kiliendelea?

Shahidi: Waliwarushia maji, mawe, marungu.

Kudushi: Uliwataja baadhi ambao uliwataja kama viongozi, walikuwa wanafanya nini?

Shahidi: Nilimuoma Freeman Mbowe akiwaamrisha wasogee mbele.

Kudushi: Na hawa viongozi wengine walikuwa wakifanya nini?

Shahidi: Wakihamasisha

Kudushi: Nini kilitokea?

Shahidi: Askari walipiga mabomu ya machozi.

Kudushi: Wakati ulipokuwa umesisima na Baba John hali ilikuaje?

Shahidi: Watu waliamua kufunga maduka yao.

Kudushi: Baada ya askari kupiga hayo mabomu ya machozi, nyie mliamua kufanya nini?

Shahidi: Tuliamua kukimbia

Kudushi: Nini kilitokea baadaye?

Shahidi: Baada ya kukimbia, tukarudi saa moja mimi nikarudi kazi kwangu, Baba John alienda kwake.

Kudushi: Ulikuta hali gani?

Shahidi: Barabara ilichafuka, kulikuwa na bendera, kulikuwa na mawe yamebaki.

Kudushi: Wewe ulivyorudi kazi, nini kiliendelea?

Shahidi: Nilibadilisha nguo, nikarudi nyumbani.

Kudushi: Na kesho nini kilitokea?

Shahidi: Tulirudi kazi kama kawaidi, tukasimuliana kilichotokea jana na kila mmoja akaendelea kufanya kazi.

Kudushi: Kuhusu wewe, nini kilitokea?

Shahidi: Hakuna kilichotokea.

Kudushi: Wewe nini kilitokea? walikuja askari walitembea kwenye fremu zote walikuwa wakipita wanasema wanatafuta ushahidi.

Shahidi: Walipofika kwangu nikatoa ushahidi jinsi inavyotakiwa wakaniambia niendeo Osterbay.

Kudushi: Osterbay wapi?

Shahidi: Polisi.

Kudushi: Nini kilifuatia?

Shahidi: Askari walisema, watanipigia simu

Kudushi: Viongozi wa Chadema uliwataja kuwa umewaona, wako wapi hapa mahakamani.

Shahidi: Wale pale (anaonesha mbele kwenye korti ya watuhumiwa).

Kudushi: Na wengine?

Shahidi: Siwafahamu

Kudushi: Unawaona kama kina nani?

Shahidi: Viongozi

Kudushi: Viongozi gani?

Shahidi: Wabunge

Itaendelea…

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!