Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Shahidi ‘ambeba’ Zitto
Habari za Siasa

Shahidi ‘ambeba’ Zitto

Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo
Spread the love

SENGWE Mbaruku, Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima (Mviwata), mkoani Kigoma amedai, Zitto Kabwe ameshtakiwa kwa sababu ya kuwasemea wananchi wa Kijiji cha Mpeta. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Shahidi huyo wa tatu kwenye kesi ya uchochezi inayomkabili Zitto ambaye ni Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, ameieleza hivyo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo tarehe 19 Machi 2020.

Awali, Sengwe aliongozwa na Jebra Kambole, wakili wa utetezi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ameieleza mahakama hiyo, kwamba amepata taarifa kupitia sehemu ya kumzika kutoka kwa mwananchi aliyetoka Kijiji cha Mpeta, kuhusu mapambano ya wananchi na polisi.

Sengwe amedai, kwamba baada ya kupata taarifa za mapambano hayo, aliziwasisha kwa baadhi ya wabunge wa Mkoa wa Kigoma akiwemo Hasna Mwilima, Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Zitto,  Mbunge wa Kigoma Mjini kuwa, polisi wanawatoa wakulima kwa nguvu na kuna mapambano kati ya wakulima na polisi.

Amedai, baada ya taarifa hiyo, Zitto alifanya mkutano na vyombo vya habari akiiomba serikali ifanye uchunguzi ili kutambua kilichokuwa kikiendelea, huku Hasna akiwasilisha suala hilo bungeni.

Wakati huo huo, wakili wa serikali mwandamizi Nassoro Katuga, amemhoji shahidi huyu juu ya ushahidi wake, amemuuliza kuhusu uelewa wake juu ya kesi aliyokuja kuitolea ushahidi, ndipo alipojibu kuwa Zitto ameshtakiwa kwa kosa la kuwasema watu wa Mpeta.

Katuga amemuuliza shahidi huyu nani aliyemuita mahakamani hapo? amedai kuwa amepigiwa simu na Zitto kuombwa aje kuieleza mahakama anachokijua kwa kile alichomwambia kuhusu mapigano ya Mpeta.

Alipoulizwa kuhusu kwenda Mpeta kwa ajili ya kujiridhisha tukio hilo, amejibu kuwa hakuweza kwenda kwa wakati huo kwa kuwa palikuwa hapaingiliki.

Wakili Katuga amemuuliza shahidi huyu kama kulitokea vurugu baada ya mkutano wa Zitto, amejibu kuwa hapakuwa na vurugu yoyote.

Awali, shahidi wa pili kwenye kesi hiyo Shabani Ally ambaye ni mwenyekiti wa ACT-Wazalendo-Kigoma Kusini, aliieleza mahakama hiyo kuwa, alishuhudi majeruhi wane kutokana na mapambano kati ya wakulima na polisi. Majeruhi hao walifikishwa katika Kituo cha Afya Nguruka.

Wakili Katuga alipomuuliza amefahamu vipi kwamba wale ni majeruhi wa mapigano? alijibu kuwa maelezo ya Dk. Sunia aliyekuwa zamu siku hiyo, ndiyo yaliyomhafahimisha suala hilo.

Ally amedai, majeruhi hao waluofikishwa kwenye Zahanati ya Nguruka usiku, asubuhi waliwaona na hakujua walienda wapi.

Ally aliitoa taarifa hiyo kwa Zitto lengo likiwa ni  Jeshi la Polisi lione kuwa, kuna tukio limetokea na wachukue hatua na kuwajibika.

Baada ya kuulizwa kama aliwahi kutoa kwenye uongizi wa serikali? amejibu kuwa aliwahi kupeleka taarifa polisi ngazi ya Wilaya kwa OCD kupitia simu. Hakimu Shahidi ameahirisha shauri hilo mpaka kesho tarehe 20 Machi 2020, asubuhi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!