Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali za Mitaa: Polisi waonya
Habari Mchanganyiko

Serikali za Mitaa: Polisi waonya

IGP Simon Sirro
Spread the love

HATUTAFUMBIA macho watu, taasisi na vyama vya siasa vitakavyokiuka sheria. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 1 Oktoba 2019 na Benedict Wakulyamba, Kamishna wa Polisi wakati akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro.

Kamishna Wakulyamba alikuwa kwenye semina ya Makamanda wa Jeshi la Polisi wa Mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani.

Kamanda Wakulyamba amesema, kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa, jeshi hilo limejipanga vyema kusimamia uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu.

Amesema, jeshi hilo halitakuwa radhi kuona mtu, taasisi au kikundi chochote kinafanya ndivyo sivyo kwenye uchaguzi huo.

“Sisi kama Jeshi la Polisi hatujaanza leo na wala hatutaacha kujipanga kikamilifu kuhakikisha shughuli hii ya uchaguzi inafanyika kwa Amani, ili kazi za serikali ziendelee bila bughudha yoyote,” amesema Kamanda Wakulyamba.

Kamanda Wakulyamba amewataka Wananchi na makundi yanayohusika na uchaguzi, kushiriki katika zoezi kwa kufuata katiba na sheria za nchi.

“Kwa niaba ya IGP, wito wetu kwa wananchi na makundi yanayohusika na uchaguzi kuwa wanashiriki zoezi hilo kwa kufuata misingi. Vyombo vinavyosimamia uchaguzi wajibu wao ni kuhakikisha suala la uchaguzi linakwenda vizuri.

Jamii pia ina jukumu la kusimamia uchaguzi unakwenda vizuri. Polisi nao wana wajibu wa kusimamia uchaguzi na kuhakikisha unakuwa mzuri,” ,” amesema Kamanda Wakulyamba na kuongeza;

“Suala la uchaguzi ni la kisiasa. Hivyo lazima lisimamiwe kwa kufuata misingi yote ya kisiasa. Ni wajibu wa kila mmoja kujua kuwa upo mfumo wa kisiasa tunaoutumia kupata viongozi wetu,” amesema Wakulyamba ambaye ni Kamishna wa Polisi, Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!