Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yawaonya watumishi, madiwani
Habari Mchanganyiko

Serikali yawaonya watumishi, madiwani

Taswila ya jiji la Mwanza
Spread the love

SERIKALI imewataka madiwani na watumishi kuacha kufanya kazi kwa mazoea ikiwemo kukubali na kufunga hoja zinazohusu namna fedha za miradi zilivyotumika kitendo kinachosababisha washindwe kuzitolea ufafanuzi, anaandika Moses Mseti.

Imesema hali hiyo imesababisha mambo mengi na ya msingi kushindwa kufanyika kwa wakati na kusababisha mkaguzi wa nje kuzikuta hoja zinazoelezea matumizi ya fedha kurundikana kuanzia miaka ya nyuma zikiwa zimeshindikana kufanyiwa utekelezaji.

Kauli hiyo imetolewa leo na Crodwing Mtweve, Katibu Tawala wa mkoa wa Mwanza, katika baraza maalumu la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Magu ambako Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za nje wa mkoani humo, Abiud Sanga (CAG) alipokuwa akitoa taarifa ya mahesabu ya halmashauri hiyo iliyopata hati safi.

“Suala la kufunga hoja bila kuzipatia ufumbuzi halitakiwi maana kumekuwepo na mambo mengi yasiyofaa katika hoja,mnayafichaficha kwa kudai hoja hizo zimeshamalizika na mkaguzi wa mahesabu akija kukagua anakutana na vitu vya ajabu.

“Pia mkiulizwa kuhusu hilo jambo, majibu yanakosekana mnabaki kurushiana mpira na nasema halmashauri yoyote (kwa mkoa Mwanza) itakayoshindwa kuzimaliza kwa kuzipatia ufumbuzi lazima iwajibishwe,” amesema Mtweve .

Abiud Sanga, Mkaguzi wa nje wa mkoa wa Mwanza, amesema katika halmashuri hiyo alibaini kuwepo kwa tatizo la manunuzi ya vifaa vya kukusanyia mapato vyenye thamani zaidi ya Sh. Milioni 14 uliyofanyika bila kukishirikisha kitengo cha manunuzi (PMU) jambo ambalo linakiuka taratibu za kazi.

Pia Sanga amesema amebaini kiasi cha Sh. 31,517,639 ambazo ni malipo ya watumishi ambao hawapo kazini bado hazijarudishwa na watumishi wanaohusika huku akidai na wapo walimu waliolipwa mishahara mara mbili Sh. 41,283,240 zilizorejeshwa zimeisha lakini halmashauri bado hawajazipeleka hazina jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Lutengano Mwalwiba, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Magu, amesema tayari walikuwa katika utaratibu wa kuzipeleka fedha hizo na juhudi za kiutendaji zimeongezeka katika ukusanyaji wa mapato ingawa kuna baadhi ya maeneo ya ushuru yameondolewa huku akiahidi kutatua changamoto hizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!