Selemani Jafo, Waziri wa Nchi ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

Serikali yataka Ma  RC ,  Ma  Dc wasijione  ‘miungu watu’

WAKUU wa Mikoa pamoja na Wakuu wa Wilaya nchini wametakiwa kutumia vizuri sheria ya kwaweka ndani watu ndani ya saa 48 na wasitumie sheria hiyo kwa kuwaonea watu, anaandika Dany Tibason.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Nchi,Ofisi ya Rais (TAMISEMI)Selemani Jaffo alipokuwa akifunga mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wao kwa lengo la kuwajengea uwezo.

Katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Uongozi, Jaffo amesema kwa sasa kuna baadhi yao  wanatumia vibaya sheria inayowapa  mamlaka ya kumuweka ndani mtu kwa  saa 48.

“Serikali imekua ikichukiwa kutokana na viongozi hawa  kutumia vibaya sheria inayompa mamkala kiongozi huyo kumuweka ndani  mtu mahabusu saa 48.

“Wapo wakuu ambao wanatumia sheria hiyo kwa kukomoana na kujifanya kuwa wao ni miungu watu bila kutambua kuwa wanapofanya hivyo wanasababisha serikali kuchukiwa bila kuwa na sababu za msingi” alisema Jafo.

WAKUU wa Mikoa pamoja na Wakuu wa Wilaya nchini wametakiwa kutumia vizuri sheria ya kwaweka ndani watu ndani ya saa 48 na wasitumie sheria hiyo kwa kuwaonea watu, anaandika Dany Tibason. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Nchi,Ofisi ya Rais (TAMISEMI)Selemani Jaffo alipokuwa akifunga mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wao kwa lengo la kuwajengea uwezo. Katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Uongozi, Jaffo amesema kwa sasa kuna baadhi yao  wanatumia vibaya sheria inayowapa  mamlaka ya kumuweka ndani mtu kwa  saa 48. “Serikali imekua ikichukiwa kutokana na viongozi hawa  kutumia vibaya sheria inayompa mamkala kiongozi huyo kumuweka ndani …

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Danson Kaijage

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube