Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Michezo Serikali yamshika mkono Babu Seya hadi studio
Michezo

Serikali yamshika mkono Babu Seya hadi studio

Familia ya Babu Seya wakiwa Ikulu kumshukuru Rais wa John Magufuli
Spread the love

SERIKALI imetangaza kuwabeba wasanii waliokuwa wamefungwa jela maisha ambao Desemba 9, 2017 walipewa msamaha na Rais John Magufuli ili kuinua vipaji vyao. Anaripoti Hamis Mguta … (endelea).

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza leo amembeba Nguza Viking aliyekuwa amehukumiwa maisha kwa kosa la ubakaji na kutembelea studio za Wanene Entertainment zilizopo Mwenge Dar es Salaaam

Babu Seya aliongozana na mwanaye Johnson Nguza ‘ Papii Kocha.

Akizungumza leo na wanahabari Shonza amesema wizara yake ambayo ina dhamana na tasnia ya muziki imeamua kwa dhati kuwasaidia wasanii hao.

“Sisi kama wizara tumeamua kuendeleza vipaji vya wasanii hawa ambao sisi ndio walezi wao, hivyo nimewasiliana na uongozi wa Wanene ambao wamekubali kushirikiana na sisi lengo ni kuhakikisha ubora wa hawa wasanii unarejea na wanafanya kazi” amesema Shonza.

Wasanii hao walipelekwa katika studio hizo na Shonza na kupokelewa na mmiliki wa Wanene, Dash ambapo walifanya mazungumzo ya pamoja yaliyolenga kurekodi nyimbo kwa wasanii hao na kusaidiwa kurudisha vipaji vyao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Piga pesa na mechi za EUROPA leo hii

Spread the love Hatimaye Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

error: Content is protected !!