Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yakiri udhaifu fomu serikali za mitaa
Habari za Siasa

Serikali yakiri udhaifu fomu serikali za mitaa

Suleiman Jafo, Waziri wa Tamisemi
Spread the love

SERIKALI imekiri kuwepo kwa udhaifu katika uchukuaji fomu, kwa ajili ya kugombea nafsi mbalimbali kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari Jumatano tarehe 30 Oktoba 2019, Seleman Jafo, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) amesema, siku ya kwanza katika uchukuaji fomu imekumbana upungufu kadhaa.

Kauli hiyo inakuja huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kikiwa tayari kimemwandikia Jafo na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kulalamikia hujuma zinazofanywa na waliopewa mamlaka ya kusimamia zoezi hilo.

Waziri huyo, amewataka waliopewa mamlaka kuhakikisha wanakabiliana na malalamiko hayo na kwamba, tayari ofisi yake imepokea malalamiko zaidi ya 70 kwa siku hiyo ya kwanza na inashughulikia malalamiko hayo.

Mapema jana, Chadema kililalamikia mazingira mabovu, vitimbi na hujuma zinazofanywa kwa wagombea wake wakati na baada ya kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi huo.

“Kufuatia matukio yanayoonesha mazingira ya kuharibu uchaguzi wa serikali za mitaa yaliyojitokeza siku ya kwanza ya kuchukua, kujaza na kurejesha fomu za uteuzi kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo, siku ya Jumanne Oktoba 29, 2019,” aimeeleza na kuongeza;

“Chadema kimemwandikia barua Waziri Jafo, kumtaka achukue hatua za haraka dhidi ya ukiukwaji mkubwa wa taratibu zinazosimamia uchaguzi huo,” alieleza Tumaini Makene, Makene, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya chama hicho.

Miongoni mwa malalamiko ya Chadema ni wasimamizi na wasaidizi wa uchaguzi kutoa nakala za fomu zisizokuwa na nembo ya halmashauri na mhuri husika, ili kuthibitisha kuwa ni nakala halisi, kutofunguliwa kwa ofisi kwa ajili ya kutoa fomu za kuomba kuteuliwa kugombea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!