Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Serikali yahaha kuzuia maandamano Australia
Kimataifa

Serikali yahaha kuzuia maandamano Australia

Spread the love

KUANZIA kesho Jumamosi tarehe 6 Juni 2020, miji mbalimbali ya Australia inatarajia kushuhudia maelfu ya raia wake kushiriki maandamano kupinga ubaguzi wa rangi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Katika mji wa New South Wales, ambapo una idadi kubwa ya watu nchini humo, leo Ijumaa tarehe 5 Juni 2020, Serikali imetinga Mahakamani Kuu kujaribu kuzuia maandamano hayo.

Maandamano hayo yanatokana na polisi wa Minnesota nchini Marekani, kumuua George Floyd, Mmarekani mweusi wiki iliyopita na kusababisha kuzuka kwa maandamano ikiwa ni siku ya tisa leo.

Hata hivyo, Scott Morrison, Waziri Mkuu wa Australian ametawaka raia wa nchi hiyo hususani wazungu, kujitenga na maandamano hayo yanayokwenda kwa jina la ‘Maisha ya Mwafrika Muhimu.’

Serikali ya nchi hiyo imekwenda mahakamani kuzuia kufanyika maandamano hayo kwa kigezo kwamba, iwapo yatafanyika yanaweza kusababisha ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19).

Waandaaji wa maandamano hayo wanaeleza kwamba, wanatarajia maelfu ya watu kushiriki maandamano hayo.

Miongoni mwa miji inayotarajiwa kushuhudiwa maandamano makubwa ni Sydney na Melbourne, kisha kuenea kwenye maeneo mwengine.

Taifa hilo, limekuwa na rekodi mbaya ya kushughulikia migogoro ya Waafrika, ambapo kuanzia mwaka 1991 mpaka sasa, watu 432 wameripotiwa kuuawa wakiwa katika mikono ya wana usalama.

Uamuzi wa maandamano hayo umepokelekwa kwa mitazamo tofauti, baadhi wamesisitiza ni muhimu kufanya hivyo licha ya tishio la kiafa huku wengine wakitaka njia nyingine itumike kuelezea hisia zao.

“Ushauri wa kiafya upo wazi kabisa, sio mpango mzuri kabisa,” Waziri Morrison amesema alipokuwa Canberra na kuongeza “Tuangalie namna nyingine kufikisha hisia zetu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaKimataifa

Faye aahidi kuongoza kwa unyenyekevu, wagombea wenzie wakubali yaishe

Spread the loveMgombea wa upinzani Senegal, Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuwa rais...

error: Content is protected !!