Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali ‘yagomea’ wapinzani bungeni
Habari za Siasa

Serikali ‘yagomea’ wapinzani bungeni

Halima Mdee, Mbunge wa Kawe, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Fedha na Mipango
Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imepingana na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kuhusu kufeli kwa hatua za Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa kuliingiza taifa katika uchumi wa kati. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Hoja hiyo iliibuliwa na Halima Mdee, Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Fedha na Mipango, bungeni jijini Dodoma Ijumaa ya tarehe 12 Juni 2020, wakati akiwasilisha maoni ya kambi hiyo kuhusu mapendekezo ya bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2020/2021.

Mdee alitoa hoja hiyo baada ya Dk. Phillip Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango, kusema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli, imejiendesha kwa mafanikio.

Katika hotuba yake, Mdee alipinga maelezo hayo ya Dk. Mpango akisema kwamba Serikali imeshindwa kujiendesha kwa mafanikio, huku akimtaka atoe ushahidi ni mahali gani serikali hiyo imefanikiwa.

Leo Jumatatu tarehe 15 Juni 2020 bungeni jijini Dodoma na Dk. Ashatu Kijaji, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, amejibu hoja ya Mdee, akisema kwamba Waziri huyo kivuli wa fedha na mipango, aliupotosha umma kwa maelezo yake kwamba Serikali imeshindwa kufikia lengo la mpango huo.

Dk. Kijaji amesema Mdee aliupotosha umma wa Tanzania kwa kuwa, lengo kuu la Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Taifa, siyo kulifikisha taifa katika uchumi wa kipato cha kati.

Naibu Waziri huyo wa Fedha amesema, lengo hilo lipo kwenye Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2020-2025.

“Hoja imepotoshwa kwa kiwango kikubwa sana, kwa hoja ya kwanza lengo kuu la mpango halikuwa kulifiksiha taifa kwenye uchumi wa kipato cha kati, hilo naomba watanzania walielewe, waziwazi ,” amesema Dk. Kijaji na kuongeza:

“Kwamba lengo la Tanzania kuwa kipato cha kati lipo kwenye Dira ya Maendeleo ya Taifa la Mwaka 2020-2025, inatekelezwa kupitia mipango mitatu ya maendeleo ya miaka mitano mitano.”

Dk. Kijaji ameeleza kuwa, lengo la Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo lilikuwa ni ujenzi wa uchumi wa viwanda, ambapo serikali hiyo imefanikiwa kutekeleza kwa asilimia 100.

“Mpango wa pili wa taifa wa a mendeleo ulioanza mwaka 2016 hadi 2021, dhima kuu ya mpango wa pili wa maendeleo ni kujenga uchumi w a viwanda ilikuchochea mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu, huo ndio mpango wa pili wa maendeleo ya watu,” amesema Dk. Kijaji.

Licha ya kufanikisha utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo, Dk. Kijaji amesema serikali hiyo pia ilifanikiwa kufikisha lengo la Mpango wa Kwanza wa Taifa wa Maendeleo, ambalo lilikuwa ni kufungua fursa fiche za ukuaji uchumi.

“Mpango wa kwanza wa maendeleo wa miaka mitano tumeuendeleza kuanzia dhima yake ikisema ni kufungulia fursa fiche za ukuaji uchumi, katika utekelezaji wa mpango wa kwanza wa maendeleo wa miaka mitano, tumeliona taifa letu likifunguka kwa miundombinu ambapo ilikuwa lengo kubwa, taifa letu linaunganishwa,” amesema Dk. Kijaji.

Dk. Phillip Mpango, Waziri wa Fedha na MIpango Tanzania

Kuhusu hoja ya hali mbaya ya kiuchumi kwa wananchi kutokana na Serikali kushindwa kutekeleza kikamilifu mpango wa huo, Dk. Kijaji amesema hoja hiyo siyo ya kweli.

Dk. Kijaji amesema hali ya wananchi kiuchumi iko vizuri, huku akitaja viashiri viwili alivyosema vinathibitisha pato la kila mwananchi linakuwa.

Kiashiria cha kwanza alichotaja Dk. Kijaji ni Tanzania kukaribia kufikia lengo la kimataifa la kila mwananchi kufikia kipato cha kati cha kuanzia dola za Marekani 1,026 hadi 3,995, ambapo kwa sasa wastani wa pato la mwananchi ni Dola za Marekani 1021.

Dk. Kijaji amesema Tanzania imebakiza dola 5 ili kufikia viwnago vya kimataifa, vya kila mwananchi kufikia pato la uchumi wa kati.

“Katika kutekeleza dhima ya mpango wa pili wa maendeleo, serikali imefanya makubwa na wanauliza tueleze Watanzania ni viashiria gani cha uchumi wa kipato cha kati ambacho taifa limefikia? nitaje viashiria viwili vya kimataifa, kiashiria cha kwanza ni wastani wa pato la mwanaanchi mmoja mmoja, “ amesema Dk. Kijaji na kuongeza:

“Pamoja na kwamba bado tuna miaka 6 ya kutekeleza Dira ya Maendeleo ya Taifa hadi mwaka 2025, sasa hivi wastani wa pato la mwananchi mmoja ni dola za marekani 1021, tumebakiza dola 5 kufika pato la uchumi wa kati.”

Kiashiria cha pili alichotaja Dk. Kijaji ni uwezo wa kutoa huduma za kijamii ikiwemo afya, elimu na maji.

“Kishiria cha pili ambacho Watanzania wameelewa naimani wapinzani ndio hawajaelewa, kiashiria kinachtolewa na Human Development Index, tunaondoka kwenye hali halisi ya utoaji huduma kwenye nchi yetu, na huduma zinazotajwa na index ziko tatu, ni uboreshaji wa huduma za afya, elimu na maji ,” amesema Dk. Kijaji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!