Naibu Waziri Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Joseph Kakunda

Serikali yagoma kuwalipa fidia waliokutwa vyeti feki kimakosa

SERIKALI  imesema hakuna mfanyakazi aliyeondolewa kazini kimakosa katika zoezi la uhakiki wa vyeti feki, zaidi ya kurudishwa kazini. Anaripoti Dany Tibason … (endelea).

Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Joseph Kakunda alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Ziwani, Nassor Suleiman Omari (CUF), aliyehoji serikali imewarejesha walimu wangapi  kazini ambao wameathirika na kukumbwa na kukutwa na vyeti feki  kimakosa.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri, Kakunda amesema kuwa ni kweli kulikuwepo na manung’uniko kwa baadhi ya watumishi wa sekta ya walimu ambao walikutwa katika mkumbo wa feti kimakosa.

Amesema kuwa walimu hao walikata rufaa na walimu wapatao 1907 walioonekana kuwa waliingizwa kimakosa katika mfumo wa vyeti feki walirudishwa kazini.

Aidha amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2016/17 na mwaka 2017/18 serikali ilifanya uhakikia wa vyeti vya watumishi wa Umma ili kubaini waliokuwa na vyeti halali na waliokuwa na vyeti vya kugushi.

Amesema katika uhakiki huo, jumla ya walimu 3,655 walibainika kuwa na vyeti vya kugushi na walipoteza sifa za kuendelea kuwa watumishi wa Umma.

Mbali na hilo amesema wale wote ambao walibainika kuwa na vyeti feki hata kama walikuwa wanakaribia kustaafu hawatalipwa mafao yoyote kwani serikali imewasemehe kuwashikati kwani watu hao walitakiwa kushitakiwa kwa kosa la jinai.

Naibu Waziri, Kakunda amesema katika harakati za kuziba pengo la walimu waliondolewa kazini, ndani ya miaka miwili serikali imeajiri jumla ya walimu 6495.

SERIKALI  imesema hakuna mfanyakazi aliyeondolewa kazini kimakosa katika zoezi la uhakiki wa vyeti feki, zaidi ya kurudishwa kazini. Anaripoti Dany Tibason ... (endelea). Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Joseph Kakunda alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Ziwani, Nassor Suleiman Omari (CUF), aliyehoji serikali imewarejesha walimu wangapi  kazini ambao wameathirika na kukumbwa na kukutwa na vyeti feki  kimakosa. Akijibu swali hilo Naibu Waziri, Kakunda amesema kuwa ni kweli kulikuwepo na manung’uniko kwa baadhi ya watumishi wa sekta ya walimu ambao walikutwa katika mkumbo wa feti kimakosa. Amesema kuwa walimu hao walikata rufaa na walimu wapatao 1907 walioonekana kuwa waliingizwa…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Danson Kaijage

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram