Serikali ya Tanzania yawaonya viongozi wa dini

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania, amewaonya viongozi wote wa dini na jumuiya za kijamii kuepuka kutoa matamko ya kisiasa yenye lengo la kuhamisha na kuelekeza waumini wao kumchagua mgombea au chama fulani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Onyo hilo, limetoka ikiwa zimebaki siku takribani saba kabla ya Watanzania kupiga kura kuwachagua madiwani, wabunge na Rais katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano tarehe 21 Oktoba 2020 na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania, George Simbachawene imesema, watakaoshindwa kutekeleza masharti, watachukuliwa hatua.

“Wiongozi watakaoshindwa kuzingatia masharti ya sheria za usajili wa jumuiya na katiba zao, wizara haitasita kuchukua hatua za kuifuta jumuiya hiyo au kutoisajili ambayo imewasilisha maombi yake,” amesema Waziri Simbachawene

Waziri huyo, amewataka viongozi hao, wazingatie sheria ya jumuiya ambayo inakataza viongozi wa kidini kujihusisha na vitendo hivyo, kwa kuwa “vinaingilia uhuru wa kikatiba wa kila mtu kumchagua mgombea anayemtaka.”

SERIKALI ya Tanzania, amewaonya viongozi wote wa dini na jumuiya za kijamii kuepuka kutoa matamko ya kisiasa yenye lengo la kuhamisha na kuelekeza waumini wao kumchagua mgombea au chama fulani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). Onyo hilo, limetoka ikiwa zimebaki siku takribani saba kabla ya Watanzania kupiga kura kuwachagua madiwani, wabunge na Rais katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Taarifa iliyotolewa leo Jumatano tarehe 21 Oktoba 2020 na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania, George Simbachawene imesema, watakaoshindwa kutekeleza masharti, watachukuliwa hatua. “Wiongozi watakaoshindwa kuzingatia masharti ya sheria za usajili wa jumuiya na…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!