SERIKALI ya Tanzania imeripoti kuwepo mgonjwa mmoja mwenye ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na Virusi vya Corona. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Taarifa ya uwepo wa mgonjwa huyo imetolewa leo tarehe 16 Machi 2020, Waziri Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, wakati akizungumza na wanahabari.
Waziri Ummy amesema mgonjwa huyo ambaye ni raia wa Tanzania, aliingia nchini tarehe 15 Machi 2020, akitokea nchini Ubelgiji kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) .
Amesema mgonjwa huyo mnamo tarehe 3 Machi mwaka huu aliondoka nchini na kwenda katika nchi za Sweden na Denmark alikokuwa kati ya tarege 5 hadi 13 Machi 2020.
“Alipowasili akafanyiwa ukaguzi na kuonekana kutokuwa na homa baadae alianza kujisikia vibaya akiwa hotelini na kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru ambapo sampuli ilipelekwa maabara ya taifa ya afya ya jamii iliyopo Dar es Salaa kwa ajili ya uchunguzi,” amesema Waziri Ummy na kuongeza:
“Vipimo vya maabara vimethibitisha kuwa mtu huyu ana maambukizi ya ugonjwa wa Corona. Mgonjwa anaendelea vizuri na matibabu.”
Waziri Ummy amewataka Watanzania kuchukua hatua juu ya janga hilo kwa kufuata ushauri unaotolewa na mamlaka za afya.
Leave a comment