SERIKALI ya Tanzania imetangaza kufuta saa 2 za nyongeza za masomo zilizokuwa zinafundishwa kila siku. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Taarifa iliyotolewa jana Jumatatu tarehe 1 Julai 2020 na Kamishna wa Elimu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania, Dk. Lyabwene Mtahaba imeelezea sababu za kuondoa saa hizo.
Mabadikiko hayo yametangazwa ikiwa ni siku chache kupita tangu Shule za Msingi na Sekondari kufunguliwa tarehe 29 Juni 2020.
Shule hizo, zilifunguliwa baada ya kufungwa kuanzia tarehe 17 Machi 2020 kutokana na kurupotiwa kwa mgonjwa wa virusi vya corona (Covid-19).
Soma zaidi:-
Kabla ya kufunguliwa, Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na waandishi tarehe 17 Juni 2020 alisema, ili kufidia muda uliopotea kutokana na mapumziko shule zitapaswa kuongeza saa 2 kila siku.
Katika taarifa ya Kamishna wa Elimu, Dk. Mtahaba imesema, imefanya tathimini na kubaini ongezeko hilo la saa 2 kila siku wamebaini haliwezekani.
“Hii ni kutokana na kuwepo kwa shule ambazo kwa sababu mbalimbali zimepewa vibali vya kuendesha masomo kwa mfumo wa ‘double shift’ na pia kutokana na tatizo la usafiri kwa wanafunzi wanaoishi mbali na shule wanazosoma,” amesema Dk. Mtahaba
“Hivyo, wizara inaelekeza shule zirejee kwenye ratiba zao za kawaida za vipindi nane kwa siku,” amesema
Dk. Mtahaba amesema, iwapo uongozo wa shule utaona kuna sababu za msingi za kuongeza muda wa taaluma basi zitumike muda uliopangwa kwenye ratiba ya Shule kwa ajili ya kutekeleza mtaala wa ziada au shughuli za nje ya Darasa.
Leave a comment