January 22, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Serikali ya Tanzania: Hatujajitenga mapambano ya corona

Prof. Abel Makubi, Mganga Mkuu wa Serikali

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imesema haijajitenga na mataifa mengine katika utafiti wa dawa na chanjo ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na virusi vya corona (Covid-19). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Prof. Abel Makubi, Mganga Mkuu wa Serikali ya Tanzania leo Jumamosi tarehe 9 Mei 2020, kufuatia malalamiko yanayotolewa na baadhi ya watu mitandaoni,  kwamba Tanzania imejitenga na mataifa ya nje, katika utafiti wa dawa na chanjo ya Covid-19.

Prof. Makubi amesema Tanzania haiwezi kujitenga na mataifa ya nje katika suala hilo na kwamba milango iko wazi kwa taifa lolote litakalohitaji kushirikiana kwenye mapambano dhidi ya Covid-19.

 “Tuko makini na hatuko hapa kufanya kazi kiholela lazima taratibu zifuatwe, hatuwezi kujitenga na nchi nyingine katika kupambana na vita dhidi ya corona, tuko wazi kwa nchi yoyote ile itakayokuwa tayari kufanya utafiti wa dawa kwa wananchi wetu,” amesema Prof. Makubi.

Prof. Makubi amesema kabla ya Tanzania kukubali kufanya majaribio ya dawa au chanjo ya Covid-19 kutoka mataifa ya nje, itazifanyia utafiti.

Amesema kwa sasa Tanzania inafuatilia dawa ya ugonjwa huo, inayotengenezwa nchini  Marekani.

“Mfano sasa hivi tunafuatilia dawa ya kutibu virusi ‘Antiviral’,  na Marekani imeonyesha mafanikio ya kutibu ugonjwa na inaweza kufanyiwa utafiti kabla ya kufanyiwa majaribio.  Lakini lazima tujiridhidhishe ubora na usalama wa hizi dawa,”  amesema Prof. Makubi.

Hadi sasa mataifa mengi hususan ya Afrika, yanaungana katika kushirikiana kutafuta dawa na chanjo ya Covid-19, ambapo Tanzania imeonyesha ushirikiano kwa nchi ya Madagascar, ambayo hivi karibuni imetangaza kupata dawa ya ugonjwa huo.

Jana tarehe 8 Mei 2020, Tanzania iliingiza nchini mitishamba inayotumika kutengeneza dawa na chanjo ya Corona-19, kutoka nchini Madagascar.

Mitishamba hiyo imeletwa nchini, baada ya Rais wa Tanzania, John Magufuli hivi karibuni kumuomba Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina, kuipatia Tanzania dawa hizo.

error: Content is protected !!