SERIKLI ya Misri kupitia Waziri wa Michezo, Ashraf Sobhy ametangaza rasmi kuwaruhusu mashabiki wa mpira wa miguu kuingia uwanjani katika michezo ya Ligi Kuu nchini humo toka walipopigwa marufuku mwaka 2012. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).
Mashabiki hao walifungiwa kuingia uwanjani toka 1 Febuari, 2012 baada ya vurugu kubwa kuibuka katika mchezo uliowakutanisha Al Masry dhidi ya Al Ahly kwenye dimba la Port Said nakupelekea mashabiki 74 kufariki dunia na wengine zaidi ya 500 kujeruhiwa.
Wapenzi hao wa soka wataanza kuingia viwanjani kuanzia tarehe 1 septemba, 2018 na kushuhudia michezo tofauti ya ligi kuu lakini waziri huyo alisisitiza watazamaji hawatakiwi kuzidi 500 kwa kila mchezo.
Ligi hiyo ya ambayo ina jumla ya timu 18 ni moja ya ligi bora na yenye ushindani kwa sasa barani Afrika, licha ya kuwa na changamoto ya baadhi ya mashabiki wake kuwa na fujo wawapo viwanjani kwenye michezo ya ndani ya ligi na hata ile ya kimataifa.
Leave a comment