Rais John Magufuli, Rais wa Tanzania. Picha ndogo Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye
Rais John Magufuli, Rais wa Tanzania. Picha ndogo Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye

Serikali ya JPM yapigwa ‘dongo’

Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye ametoa tuhuma nzito kwa serikali ya awamu ya tano huku akisema kuwa haizingatii misingi ya sheria pamoja na kuheshimu utawala bora, anaandika Hellen Sisya.

Amesema serikali ya awamu ya tano imeshindwa kuheshimu mhimili wa Mahakama pamoja na Bunge na kwamba Mahakama Kuu ilitoa zuio la muda katika kumpora mashamba yake lakini, amri hiyo imepuuzwa.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika mapema leo hii katika ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kanda ya Pwani, zilizopo eneo la Magomeni jijini Dar es salaam, Sumaye amesema serikali imempokonya mashamba yake pasipo kujali zuio ambalo Mahakama Kuu.

“Kama nilivyokwisha eleza, tulifungua kesi mbili Mahakama Kuu kwa kufuata taratibu zote za kisheria, moja dhidi ya wavamizi na nyingine dhidi ya serikali”, amesema Sumaye

Mwanasiasa huyo amefafanua kuwa kesi ziko mahakamani na zinaendelea hata sasa na mahakama imeweka zuio la muda kwa shughuli yoyote kutoendelea katika eneo hilo na wahusika wote yaani wavamizi na serikali wana taarifa hiyo.

Sumaye ameweka wazi kwamba shamba hilo limetwaliwa na rais kwa maagizo ya kuligawa kwa wananchi huku ikidaiwa kwamba wavamizi wapewe kipaumbele.

Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn
WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye ametoa tuhuma nzito kwa serikali ya awamu ya tano huku akisema kuwa haizingatii misingi ya sheria pamoja na kuheshimu utawala bora, anaandika Hellen Sisya. Amesema serikali ya awamu ya tano imeshindwa kuheshimu mhimili wa Mahakama pamoja na Bunge na kwamba Mahakama Kuu ilitoa zuio la muda katika kumpora mashamba yake lakini, amri hiyo imepuuzwa. Katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika mapema leo hii katika ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kanda ya Pwani, zilizopo eneo la Magomeni jijini Dar es salaam, Sumaye amesema serikali imempokonya mashamba yake pasipo kujali zuio ambalo…

Review Overview

User Rating: Be the first one !
0

About Hellen Sisya

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube