Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali waikataa barua yao kwenda KKKT
Habari za SiasaTangulizi

Serikali waikataa barua yao kwenda KKKT

Spread the love
MWIGULU Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, amekanusha kuwa barua iliyoandikwa na wizara hiyo ya kulitaka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) kuufuta waraka wa Pasaka ni batili na siyo maelekezo ya serikali au wizara. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

“Tunawaomba viongozi wa dini waendelee na kazi zao, nasema jamii iwe macho na taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya jamii na wasifanyie kazi taarifa hizo,” amesema.

Kadhalika, Dk Nchemba amesema amefuatilia barua hizo na kuona zina mkanganyiko wa anuani.

“Viongozi wa dini wasiwe na taharuki na taarifa hizo, hazina baraka za Serikali. Wasisite kuwasiliana na Serikali kujua uhalali wake.” Amesema.

Pia Dk Nchemba amesema waraka wa viongozi wa dini uliotolewa miezi iliyopita ni jambo lililopita na hivyo akawataka viongozi wa dini waendelee na kazi zao.

Dk Nchemba amewataka viongozi wa dini kuendelea na kazi zao. “Nchi yetu ni moja na tunaishi kwa taratibu tulizojiwekea na tuna madhehebu mengi.” Amesema na kuongeza: “Wengine wameliona jambo hilo kama ajenda. Wananchi wawe makini, wasiwafuate watu hao wanaotaka kuwagawa.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!