Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali kuvuna Bil 418 za korosho
Habari Mchanganyiko

Serikali kuvuna Bil 418 za korosho

Spread the love

SERIKALI imeanza kuingia mkataba wa mauzo ya korosho na wafanyabiashara ambapo tayari jumla ya tani 100,000 za zao hilo zimepata mteja. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kampuni ya Indopower Solutions ya Kenya ikiwakilishwa na Brian Mutembei, ofisa mtendaji mkuu wake ameingia mkataba wa mauzo ya korosho na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko, Hussein Mansoor.

Wawakilishi hao wawili waliingia mkataba wa ununuzi wa tani 100,000 za korosho walipokutana kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi za Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jijini Dar es Salaam tarehe 30 Januari 2019.

Shughuli hiyo ilishuhudiwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi; Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda; Gavana wa Benki Kuu (BoT), Prof. Florens Luoga; Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa.

Kwenye hafla hiyo Prof. Kabudi amesema kuwa, serikali itavuna Sh. 418 bilioni pale fedha hizo zitakapoingia BoT na kwamba, Rais Magufuli alifanya uamuzi sahihi wa kununua korosho zote kutoka kwa wakulima na kusaka mnunuzi mkubwa.

Awali Kasim Majaliwa, Waziri Mkuu aliwatoa hofu wananchi hususan wakulima wa korosho nchini baada ya kuwahakikishia kuwa, korosho zao zote zitanunuliwa na serikali.

Amesema Serikali kupitia Bodi ya Mazao Mchanganyiko itanunua korosho zote na hakuna korosho za wakulima nchini ambazo zitabaki bila ya kununuliwa.

Kutokana na vuta nikuvute kuhusu ununuzi wa zao hilo na bei elekezi, Rais Magufuli baada ya kutoridhishwa na namna wateule wake walivyosimamia, tarehe 10 Novemba 2018aliwafuta kazi Dk. Charles Tizeba wa Wizara ya Kilimo na Dk. Charles Mwijage wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Pia Rais Magufuli alivunja Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) na kutengua uteuzi wa mwenyekiti wa bodi hiyo, Anna Abdallah.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!