Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Serikali kuingia mgogoro na Marekani?
KimataifaTangulizi

Serikali kuingia mgogoro na Marekani?

Prof. Palamagamba Kabudi
Spread the love
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano, yaweza kujiingiza kwenye mgogoro mwingine wa kidplomasia na mataifa ya Magharibi, kufuatia uamuzi wake wa kumpokea na kumruhusu kufanya kazi nchini, Anselem Nhamo Sanyatwe. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Sanyatwe, ni miongoni mwa maofisa wa serikali ya Zimbawe wanaotuhumiwa na mataifa ya Magharibi na Marekani, kuhusika na mauwaji ya raia nchini humo. Ameteuliwa na nchi yake kuwa balozi wake nchini Tanzania.

Serikali ya Marekani kupitia wizara yake ya mambo ya nje, imetangaza vikwazo dhidi ya Sanyatwe. Taarifa ya wizara hiyo imesema, ina taarifa za kuaminika kuwa Sanyatwe alihusika katika mauaji ya raia wa Zimbabwe yaliyotokea 1 Agosti 2018.

Senyatwe alikuwa Brigedia wa jeshi la kitaifa la ulinzi wa rais. Mauaji hayo yalitokea kufuatia ghasia zilizozuka kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2018. Makumi ya watu waliuawa.

Serikali ya Rais Donald Trump imesisitiza, “Bregidia Sanyatwe, ni mmoja wa wahusika wakuu wa mauaji ya raia na ukatili dhidi ya binadamu nchini mwake. Serikali mjini Washington DC, imejiridhisha kuwa Sanyatwe ni mkosaji anayepaswa kufikishwa mahakama.”

Kuibuka kwa taarifa kuwa Marekani imempiga marufuku Brigedia Sanywate anayewakilisha nchi yake nchini na kumuwekea vikwazo, kumekuja katika kipindi ambacho uhusiano kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia (WB), umekuwa siyo nzuri.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, WB imezuia takribani dola za Marekani 1.3 trilioni kwa Tanzania. Fedha hizo zilipangwa kutumika kwenye miradi ya maendeleo, ikiwamo kuboresha elimu ya sekondari na kusaidia kaya masikini.

MwanaHALISI ONLINE halikuweza kumpata Prof. Paramagamba Kabudi, waziri wa mambo ya nchi za nje na uahirikiano wa Afrika Mashariki, kueleza msimamo wa serikali kufuatia uamuzi huo wa Marekani kumuwekea vikwanzo balozi huyo wa Zimbabwe.

Anselem Nhamo Sanyatwe

Ghasia za uchaguzi nchini Zimbabwe zilibuka tume ya uchaguzi kumtangaza Emmerson Mnangagwa kutoka ZANU-PF kuwa mshindi dhidi ya mgombea wa chama cha Movement for Democratic Change (MDC).

Magari yaliobeba maji na vitoa machozi yalitumika kuwatawanya waandamanaji katika barabara muhimu za mji wa Harare baada ya wafuasi wa MDC kuweka vizuizi katikati ya mji huo.

Chama cha upinzani cha muungano wa MDC kilisema kwamba kura za wananchi zilifanyiwa udanganyifu na kwamba mgombea wake Nelson Chamisa alikuwa ameibuka mshindi.

Serikali ya Zimbabawe imeleza kutofurahishwa kwake na hatua hiyo ya Marekani kumuekea vikwazo Balozi Brigedia Sanyatwe. Serikali mjini Harare imesema, hatua hiyo ya Marekani, ni kuingilia uhuru wake.

Kwa mujibu wa mkataba wa umoja wa mataifa – Vienna Convention on Diplomatic Relations of 1961 – pamoja na kwamba mabalozi wana kinga ya kukamatwa na kuwekwa kizuizini katika nchi wanapofanyia kazi, lakini Ibara ya 41 inaeleza kuwa hadhi ya ubalozi haiwezi kutumika kinyume na Sheria ya Kimataifa (International Law). 

Hatua ya serikali kuendelea kumtambua na kumruhusu kufanya kazi nchini, Brigedia Senywate, ni kinyume na mkataba huo wa Vienna na hivyo kuifanya Tanzania kumulika na mataifa mengi duniani, hasa yale yanayoheshimu utawala bora.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

Habari za SiasaTangulizi

CAG aibua madudu halmashauri 10, TANESCO na MSD

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!