Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali haijui athari za soko la Afrika Mashariki
Habari za SiasaTangulizi

Serikali haijui athari za soko la Afrika Mashariki

Dk. Ashatu Kijaji, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
Spread the love

SERIKALI imesema inafanya tathimini ili kujua athari ilizopata Tanzania kufuatia hatua yake ya kufungua masoko yake yote kwa pamoja katika soko la pamoja la Afrika Mashariki, kisha kuiwasilisha bungeni. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji kwa niaba ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, wakati akijibu swali la Mbunge wa Nkenge, Balozi Diodorus Kamara.

“Kuhusu tathimini ya athari za kufungua maeneo yote katika soko la pamoja, serikali inafanya tathimni ili kujua na itakapokamilika bunge lako tukufu itapata tathimini ya athari hizo,” amesema Dk. Kijaji.

Katika swali lake la nyongeza, Balozi Kamara alihoji kuwa, kutokana na Tanzania kuchelewa kufungua soko na kwamba hivi karibuni imefungua masoko yake yote katika soko la pamoja la jumuiya ya Afrika Mashariki, je imepata athari gani kufuatia hatua yake hiyo.

“Kwa kuwa soko la pamoja hadi sasa lina wastani wa miaka nane, kwa kuwa Tanzania wakati tunajadiliana kuanzisha soko la pamoja tulichelewa kufungua soko letu na sasa tumefungua karibuni yote, kama tumefanya tathimini ya athari ya kufungua masoko yote, ningefurahi kupata nakara hiyo kama imefanyika,” amesema Balozi Kamara.

Vile vile, Balozi Kamara amehoji mkakati wa serikali katika kuongeza idadi ya Watanzania wanaonufaika na soko la ajira katika jumuiya hiyo, na kujibiwa na Dk. Kijaji aliyesema kwamba serikali imejipanga kuimarisha mifumo ya elimu ili Watanzania wakidhi vigezo vya kupata ajira, huku akiwataka kuomba ajira pindi fursa zitakapotangazwa.

Kuhusu mafanikio ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Dk. Kijaji amesema uanzishwaji wa jumuiya hiyo umesaidia kuongezeka kwa fursa za kibiashara, kupunguzwa vikwazo vya kibiashara kwa wananchi wa nchi mwanachama ambapo mwaka 2010 vilikuwa 158 hadi kufikia 31 mwaka 2018 pamoja na wananchi wa nchi mwanachama kuwa huru kutembelea nchi za jumuiya hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

Habari za SiasaTangulizi

CAG aibua madudu halmashauri 10, TANESCO na MSD

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!