Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali: Bei ya korosho ni 3,300 – 2,640
Habari za Siasa

Serikali: Bei ya korosho ni 3,300 – 2,640

Zao la Korosho
Spread the love

SERIKALI ya Jamhuri imeeleza kuwa, bei inayotumika kununua korosho za wakulima ni Sh. 3,300 kwa zile za gredi ya kwanza na 2,640 kwa korosho za gredi ya pili. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo imetplewa leo bungeni tarehe 4 Februari 2019 na Omar Mgumba, Naibu Waziri wa Kilimo na kwamba, korosho zilizo chini ya kiwango hicho hazitanunuliwa.

Mgumba amesema kuwa, serikali haiwezi kununua korosho ambazo ni ‘mawe’ ili kuondokana na kushusha thamani kama vitendo mbavyo viliwahi kutokea awali na kusababisha zao hilo kuonekana halina thamani.

Kauli hiyo imetolewa baada ya Cecil Mwambe, Mbunge wa Ndanda (Chadema) kuitaka serikali itoe kauli ni kwanini imekuwa hainunui korosho kwa bei elekezi ya Rais John Magufuli.

Mbunge huyo alihoji serikali na kutaka ieleze kuwa, kuna tofauti gana ya wanunuzi wa korosho kwa mtindo wa Kangomba kwa wanunuzi wadogo na wanaunuzi wa Kangomba kwa wanaunuzi wakubwa kutoka nchi za nje.

Awali katika swali la Halima Mdee, Mbunge wa Jimbo la Kawe (Chadema) alisema kuwa, mwezi  Novemba 2018  rais aliutangazia ulimwengu kwamba serikali yake itanunua korosho  zote kwa bei isiyopungua shilingi 3000.

Kutokana na kauli hiyo ya rais Mdee alitaka kujua mpaka sasa ni kiasi gani kimetumika na kutoka chanzo kipi na je tani ngapi zimenunuliwa.

Mgumba amesema, kuhusu kangomba alisema serikali haifanyi biashara hiyo bali inanunua korosho na kuuzia kampuni kubwa ambazo zipo tayari kununua zao hilo.

Aidha Naibu Waziri huyo alisema kuwa katika makadirio ya uzalishaji wa korosho msimu wa 2018/2019 ni zaidi ya tani 240,000 za korosho ghafi.

Amesema, hadi kufikia Januari 30, mwaka huu serikali imenunua jumla ya tani 214,269,684 za korosho ghafi zenye thamani ya Sh.707,089,957,200 sawa na asilimia 89.3 ya leno la uzalishaji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!