Thursday , 18 April 2024
Home Kitengo Michezo Serengeti Boys yafuzu fainali za Vijana
Michezo

Serengeti Boys yafuzu fainali za Vijana

Kikosi cha timu ya Taifa ya vijana chini umri wa miaka 17, Serengeti Boys
Spread the love

HATIMAYE timu ya Taifa ya vijana chini umri wa miaka 17, Serengeti Boys imefuzu kucheza michuano ya kombe la mataifa Afrika baada ya kushinda rufaa walioiweka dhidi ya mchezaji wa timu ya taifa ya Jamuhuri ya Congo, Langa Lesse Bercy kutokana na umri wake.

Congo hapo awali ilifuzu michuano hiyo baada ya kuitoa timu ya Serengeti Boys kwa kuifunga bao moja kwa bila katika mchezo wa marudiano uliofanyika Kinshasa, licha ya Tanzania kushinda mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza uliofanyika jijini Dar es salaam.

Kamati ya utendaji ya CAF iliyokaa mjini Libreville, nchini Gabon imeipa ushindi Tanzania, baada ya timu ya Jamhuri ya Congo kumchezesha mchezaji Langa Lesse Bercy aliyezidi umri kinyume na kanuni za michuano hiyo.

Katika kipindi cha nyakati tofauti, CAF walitoa agizo la kwa shirikisho la soka la Jamhuri ya Congo (FECOFOOT) kumpeleka kijana huyo Cairo, Misri kwa ajiri ya vipimo vya MRI iliwaweze kujilidhisha juu ya tuhuma hizo lakini Congo hawakulifanya hilo

Fainali hizo zinatarajia kufanyika Aprili 2, mwaka huu katika nchi ya Gabon, ambao wameandaa fainali za kombe la mataifa Afrika mwaka huu, baada ya CAF kuiengua Madagascar kuandaa fainali hizo kutokana kutojilidhisha namna ya maandalizi yalivyokuwa yanafanyika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

Michezo

TFF, Amrouche ngoma nzito

Spread the loveVIPENGELE vya mkataba wa kazi aliotia saini Kocha Mkuu wa...

error: Content is protected !!