Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Michezo Serengeti Boys kutinga Bungeni Kesho
Michezo

Serengeti Boys kutinga Bungeni Kesho

Kikosi cha timu ya Taifa ya vijana chini umri wa miaka 17, Serengeti Boys
Spread the love

Timu ya Taifa ya Vijana chini ya Umri wa Miaka 17, ‘Serengeti Boys’ ikiongozwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Jamal Malinzi imeondoka leo kuelekea bungeni Dodoma, baada ya kupata mwaliko kutoka kwa Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Serengeti boys imepata mualiko huo baada ya kufanikiwa kufuzu kwenye fainali za kombe la mataifa Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, ambazo zinatarajia kuanza Mei 21, mwaka huu nchini Gabon.

Timu hiyo ambayo inatarajia kuweka kambi ya mwezi mmoja nje ya nchi kabla ya kuelekea Gaboni, ili kuweza kupata muda mrefu wa maandalizi licha ya kukabiliwa na changamoto kubwa ya kifedha kwa sasa kutokana na timu hiyo ya Vijana kutokuwa na mdhamini kwa sasa.

Licha ya Serengeti boys kuitikia wito huo na kuhudhulia baadhi ya vikao vya bunge vinavyoendelea huko Dodoma kesho, lakini timu hiyo hapo awali ilipokea barua ya pongezi kutoka kwa Spika wa Bunge baada ya kufanikiwa kucheza michuano.

Wajumbe wengine waliongozana na Vijana hao kwenda Bungeni Dodoma, ni Ayoub Nyenzi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Mpira wa Miguu kwa vijana, Mulamu Ng’ambi Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma (DOREFA), Salum Madadi, Alfred Lucas Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Kim Poulsen amabaye ni Mshauri wa Ufundi wa Soka la Vijana na wengine ni .Mwarami Mohammed na Edward Venance.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Tusua mkwanja na mechi za Ijumaa leo

Spread the love  LEO hii mechi zinaendelea kote na wewe kama unataka...

Michezo

Piga pesa na mechi za EUROPA leo hii

Spread the love Hatimaye Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

error: Content is protected !!