NAIBU Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sheikh Naim Qassim amesema kuwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia inaonesha kukiri kushindwa kwake baada ya kukubali kuanzishwa maeneo ya kupunguza mivutano nchini Syria, anaandika Jovina Patrick.
Jumapili ya jana Adel al-Jubeir, Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia akizungumza na waandishi wa habari nchini humo ikiwa ni miaka sita ya vita na baada ya kushindwa makundi ya kigaidi kwa ajili ya kuiondoa madarakani serikali ya Damascus, alisema kuwa Saudia inakubaliana na pendekezo la kuanzishwa maeneo ya kupunguza mizozo nchini humo.
Lengo kuu la mazungumzo hayo ni kutiwa saini makubaliano yenye lengo la kuanzishwa maeneo ya kupunguza migogoro nchini Syria. Kufuatia hali hiyo Sheikh Naim Qassim akizungumza na kanali ya televisheni ya al-Manar amesema kuwa, Saudia inapitia wakati na kipindi kigumu kutokana na kushindwa mipango yake yote katika eneo la Mashariki ya Kati.
Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, muqawama nchini Syria umekuwa ukisajili ushindi na kwamba ushindi huo utaendelea
Ameongeza kuwa, kukombolewa mji wa Aleppo kumefelisha njama za maadui za kutaka kuigawa vipande nchi ya Syria na kwamba kukombolewa mji wa Deir ez-Zor, ni ushindi mwingine mkubwa dhidi ya genge la kigaidi la Daesh.
Leave a comment