Sasa naomboleza kifo cha mama – kabendera

Spread the love

ERICK Kabendera, mwandishi wa habari za uchunguzi ndani na nje ya nchi, amesema ‘sasa naomboleza kifo cha mama yangu.” Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).

Kabendera ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kuachwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, tangu tarehe 5 Agosti 2019 alipokuwa akishikiliwa kwa makosa ya matatu likiwemo la utakatishaji fedha.

Mama yake Kabendera, Verdiana Mjwahuzi alifariki dunia tarehe 31 Desemba 2019 na kuzikwa tarehe 4 Januari 2020, mkoani Kagera.

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 24 Agosti 2020, baada kuachiwa huru kwa kulipa faini ya Sh. 250,000 na Sh. 100 milioni baada ya kuamriwa na mahakama, Kabendera amesema atakutana na watu wachache walimfariji tangu akumbane na mkasa huo.

Pia amewashukuru wanahabari wenzake wanaharakati, watu wa kada mbalimbali na Watanzania wote kwa kuwa naye karibu wakati akiwa kwenye matatizo.

Kabendera ameondoka na ndugu zake kwenye viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi saa 10 alasiri.

ERICK Kabendera, mwandishi wa habari za uchunguzi ndani na nje ya nchi, amesema ‘sasa naomboleza kifo cha mama yangu.” Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea). Kabendera ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kuachwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, tangu tarehe 5 Agosti 2019 alipokuwa akishikiliwa kwa makosa ya matatu likiwemo la utakatishaji fedha. Mama yake Kabendera, Verdiana Mjwahuzi alifariki dunia tarehe 31 Desemba 2019 na kuzikwa tarehe 4 Januari 2020, mkoani Kagera. Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 24 Agosti 2020, baada kuachiwa huru kwa kulipa faini ya Sh. 250,000 na Sh. 100 milioni baada ya…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Hamisi Mguta

One comment

  1. Great content! Super high-quality! Keep it up! 🙂

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!