Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Saratani ya matiti yaanza kushambulia wenye umri mdogo
Habari Mchanganyiko

Saratani ya matiti yaanza kushambulia wenye umri mdogo

Dk. Crispian Kahesa, Mkurugenzi wa Huduma za Kinga ya Saratani katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI)
Spread the love

WASTANI wa umri wa wanawake wanaogundulika kuugua saratani ya matiti katika Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) umeshuka. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam… (endelea).

Takwimu zinaonesha mwaka 2008/09 wanawake waliokutwa wakiugua saratani hiyo walianzia miaka 64 lakini mwaka 2019 walianzia miaka 56.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa ORCI, Dk. Crispin Kahesa alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu Mwezi Oktoba ambao ni maalum kwa ajili ya uhamasishaji na uelimishaji juu ya saratani hiyo duniani.

Kwa mujibu wa Dk. Kahesa, takwimu hizo zinaonesha wazi hali hiyo ni kiashiria cha hatari kwamba saratani hiyo sasa imeanza kushambulia hadi wanawake wenye umri mdogo tofauti na miaka ya nyuma.

“Umri wa miaka 56 ni wastani ambao tumeupata baada ya kujumlisha data zetu, wapo hadi wanawake wenye umri kuanzia miaka 25 ambao tumewakuta na saratani hii, hapa kwenye taasisi yetu,” amesema Dk. Kahesa.

Aidha, kupitia takwimu za Taasisi ya Globalcan za 2018, inakadiriwa zaidi ya wagonjwa 42,060 wa saratani ambao hugundulika kila mwaka Tanzania na kati ya hao asilimia 7.2 ni wa saratani ya matiti.

“Katika uhalisia, takwimu zetu nchini zinaonesha mwaka 2018 wagonjwa wa saratani walioweza kuhudhuria hospitalini ni zaidi ya 12,215 kati ya hao 42,060 wanaokadiriwa.

“Aidha, kati ya hao 12,215 walioweza kuhudhuria wanawake waliopata saratani ya matiti walichukua wastani wa asilimia 16 ya wagonjwa wote,” amesema.

Ameongeza “Hapa Ocean Road ambako tunapokea wagonjwa kutoka nchi nzima mwaka 2018/19 tuliona zaidi ya wagonjwa 7,426 kati ya hao 965 walikuwa wa saratani ya matiti ambao ni wastani wa asilimia 13.

Hata hivyo takwimu za ORCI zinaonesha saratani ya matiti ni tatizo kubwa ikishika nafasi ya tatu kwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa, baada ya saratani ya kizazi na saratani ya tezidume.

Takwimu zinaonesha kuna hatari ya wanawake 17 katika kila wanawake 100,000 kupata saratani hiyo, kibaya zaidi kati ya wanawane 100,000 wanawake 22 hupoteza maisha kutokana na saratani hiyo.

Kutokana na hali hiyo Dk. Kahesa amesema katika kuadhimisha mwezi huo wa Oktoba, wataalamu wa taasisi hiyo wamejipanga vema kutoa elimu kwa jamii kuhusu saratani hiyo pamoja na kufanya uchunguzi wa awali ili kuwagundua mapema wagonjwa.

“Kwa kuwa tunaona wenye umri mdogo nao wanagundulika hivi sasa, tunakusudia kuwafikia moja kwa moja, tutaanza na vyuo viwili (tutavitaja baadae sasa wapo kwenye mitihani) na hapa ORCI elimu na uchunguzi wa awali unaendelea kufanyika,” amebainisha.

Saratani hiyo inaelezwa kuathiri jinsi zote lakini kwa wanaume ni kwa kiwango kidogo cha asilimia moja tu kwa wanawake ni asilimia 99.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!