Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Samia awabebesha ‘zigo’ SIDO
Habari Mchanganyiko

Samia awabebesha ‘zigo’ SIDO

Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Tanzania
Spread the love

SAMIA Suluhu, Makamo wa Rais wa Tanzania ameliagiza Shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo nchini (SIDO) kuhakikisha linasimamia viwanda hivyo vinavyoanzishwa na watumishi wa umma pindi wanapostaafu, anaandika Moses Mseti.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati wa semina kwa wastaafu watarajiwa wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF mkoa wa Mwanza, uliohudhuliwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa akiwemo Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Ashatu Kijazi.

“Kufanya hivyo kutasaidia viwanda vidogo vinavyoanzishwa na watumishi wanao staafu na watu binafsi nchini kuweza kuchangia katika ukuaji wa maendeleo na kuongeza pato la taifa,”amesema Samia.

Kutokana na PSPF kutarajiwa kuwalipa wastaafu 9, 552 kiasi cha Bilioni 1.3 nchi nzima, amesema ni vyema elimu ikatolewa kwa wastaafu watarajiwa ili fedha hizo zitumike kwa shughuli za maendeleo.

Samia alisema kuwa baada ya elimu hiyo kutolewa, watumishi wanapostaafu ni bora wakawekeza katika sekta ya viwanda vidogo ambao ndio msingi mkubwa wa Viwanda vya kati na vikubwa.

“Ifikapo mwaka 2025 Tanzania tunatarajia kufika katika uchumi kati, lazima tuanze kuwekeza katika viwanda vidogo vidogo, kwa kuwekeza kwenye kilimo, biashara na ufugaji na hiyo ni kwa kuweka mpango mzuri kwa wastaafu ukawekwa,” amesema Samia.

Katika hatua hiyo, makamo wa rais amewataka watumishi wanaotarajiwa kustaafu na wanaostaafu kuacha matumizi mabaya ya fedha pindi wanapostaafu ikiwemo kuacha kuowa mabinti wadogo.

Amesema kuwa hali hiyo, imekuwa ikisababisha kuendelea kuwepo kwa wastaafu masikini na kwamba hali hiyo imekuwa ikiwasababishia kuishi kwa shida na kuwa na msongo wa mawazo.

Ashatu Kijazi, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, amesema semina hiyo ni nzuri na kwamba itasaidia wastaafu hao watarajiwa kupata elimu na kwamba pindi watakapo staafu  watakwenda kutengeneza ajira kwa vijana nchini.

Adam Mayingu, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, amesema PSPF unahudumia wanachama 403, 605 na wastaafu tegemezi 62, 892 huku akidai tangu mfuko uanze umelipa wastaafu kiasi cha trioni 4.2  na kwamba wameamua kutoa mafunzo kwa watumishi hao kwa lengo la kuwaongezea uwezo ili wanapostaafu waweze kutumia vizuri fedha wanazopewa.

Mayinga amesema kuwa kwa mwaka wa fedha wa 2017/ 18 unatarajiwa kuwalipa wanachama 9, 552 ya mafao kiasi cha Bilioni 1.3 huku akidai kiasi hicho ni kikubwa lazima elimu itolewe namna ya kupanga maisha yao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!