Samatta: Nawashukuru Aston Villa, nimetimiza ndoto zangu

Spread the love

NAHODHA wa timu ya soka ya Tanzania ‘Taifa stars’ Mbwana Samatta ameishukuru timu ya Aston Villa kwa kumwezesha kutimiza ndoto zake za kucheza LIgi Kuu ya Uingereza (EPL). Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Samatta aliyejiunga na Aston Villa Januari 2020 kwa mkataba wa miaka minne na nusu akitokea KRC Genk ya Ubelgiji, leo Ijumaa tarehe 25 Septemba 2020 ametangazwa na timu ya Fenerbahce ya Uturuki kuwa mchezaji wake mpya.

Tayari Samatta ameanza mazoezi na timu yake mpya inayoshiriki Ligi Kuu ya Uturuki.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Samatta akiwa Aston Villa alicheza michezo 16 na kufunga magoli mawili, amewashukuru timu nzima na mashabiki kwa ushirikiano waliompa.

“Naishuruku Aston Villa kwa kunipa nafasi ya kufikia ndoto zangu za kucheza Ligi Kuu ya Uingereza.”

“Shukrani za kipekee ziwafikie mashabiki wote wa Aston Villa kwa ushirikiano walionipa katika kipindi chote nikiwa na Villa. Nawatakia kila la kheri,” amesema Samatta

NAHODHA wa timu ya soka ya Tanzania ‘Taifa stars’ Mbwana Samatta ameishukuru timu ya Aston Villa kwa kumwezesha kutimiza ndoto zake za kucheza LIgi Kuu ya Uingereza (EPL). Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea) Samatta aliyejiunga na Aston Villa Januari 2020 kwa mkataba wa miaka minne na nusu akitokea KRC Genk ya Ubelgiji, leo Ijumaa tarehe 25 Septemba 2020 ametangazwa na timu ya Fenerbahce ya Uturuki kuwa mchezaji wake mpya. Tayari Samatta ameanza mazoezi na timu yake mpya inayoshiriki Ligi Kuu ya Uturuki. Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Samatta akiwa Aston Villa alicheza michezo 16 na kufunga magoli mawili, amewashukuru timu nzima na…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

One comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!