Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Safu ‘nzuri ACT-Wazalendo
Habari za SiasaTangulizi

Safu ‘nzuri ACT-Wazalendo

Maalim Seif Shariff Hamad akikabishiwa kadi alipojiunga na ACT-Wazalendo
Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimepata viongozi wa juu wawili, walioridhiwa na wanachama wa chama hicho usiku wa manane kuamkia leo tarehe 15 Machi 2020. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea).

Kwenye uchaguzi huo ulioana jana mchana tarehe 14 Machi 2020 na kumalizika saa 9 usiku, Maalim Seif Shariff Hamad amechaguliwa kuwa mwenyekti mpya wa chama hicho huku Zitto Kabwe, akiendelea kuwa kiongozi mkuu kwa mara ya pili.

Maalim Seif alipata kura amepata kura 337 sawa na asilimia 93.30 ambapo aliyemfuata Yeremia Kulwa Maganja amepata kura 20 swa na asilimia 5.55  huku Shilingushela Kahesa Nyangaki akipata kura 4 sawa na asilimia 1.01ambapo kura zilizoharibika zilikuwa mbili.

Kabla ya uenyekiti, Maalim Seif alikuwa Mshauri Mkuu wa wa chama hicho. Uchaguzi huo umeridhiwa na wajumbe wa mkutano huo kwamba ulikuwa huru, uwazi na haki.

Wakati akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Omar Said Shabaan ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Uchaguzi wa ACT-Wazalendo amesema, jumla wajumbe walioshiriki mchakato huo ni 375, kura halali zilikuwa 367 na zilizoharibika nane.

“Kwa matokeo haya nikiwa mwenyekiti wa kamati maalumu ya uchaguzi namtangaza kwenu Maalim Seif kuwa mwenyekiti wa ACT -Wazalendo,” amesema Shabaan huku wajumbe wa mkutano huo wakishangilia.

Katika nafasi ya kiongozi mkuu wa chama hicho, Zitto amepata kura 276 sawa na asilimia 73.6 wakati Ismail Jussa amepata kura 91 sawa na asilimia 24.2.

Uchaguzi huo unaendelea leo katika nafasi mbalimbali ikiwemo Makamu Mwenyekiti, wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Kamati Kuu ya Chama ambapo kesho wajumbe watakaopatikana kesho watapiga kura ya kumchagua Katibu Mkuu wa chama na manaibu wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!