Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sababu za wanawake kuota ndevu, wanaume matiti zatajwa bungeni
Habari za SiasaTangulizi

Sababu za wanawake kuota ndevu, wanaume matiti zatajwa bungeni

Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalum, Zainab Mndolwa ameitaka serikali kufanya utafiti kuhusu madai ya baadhi ya wanawake kuota ndevu na wanaume kuota maziwa kutokana na kula nyama na mayai ya kuku wa kisasa. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Mndolwa ametoa wito huo leo tarehe 16 Novemba 2018 bungeni jijini Dodoma, ambapo amedai kuwa, ufugaji wa kuku wa kisasa hutumia dawa nyingi zinazopelekea kuku hao kukua ndani ya muda mfupi, na kutaka kujua athari za dawa hizo kwa afya ya binadamu.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo, Abdallah Ulega amesema hakuna utafiti wa kisayansi unaothibitisha madhara yatokanayo na ulaji wa nyama na mayai ya kuku wa kisasa, hata hivyo amesema serikali itajikita kufanya utafiti ili kujua ukweli wa madai hayo.

Ulega amewatoa wasiwasi Watanzania akisema kuwa, ulaji wa nyama na mayai ya kuku wa kisasa hauna madhara, na kwamba serikali inaendelea kusimamia usajili na utengenezaji wa vyakula vya kuku wa kisasa ili viwe na ubora na kupunguza usambazwaji wa vyakula vyenye vimelea vya ugonjwa.

“ Napenda kulijulisha bunge lako tukufu kwamba ulaji wa nyama za kuku wa kisasa au mayai hauna madhara, ufugaji wa kisasa hauendani na dawa nyingi kama ilivyoelezwa katika swali la msingi, chakula kinazotumika na chanjo sio dawa, ni virutubisho na hakuna madhara kwa afya ya binadamu, kukua kwa muda mfupi ni kutokana na ubora wa lishe, na si matumizi ya dawa,” amesema na kuongeza Ulega.

“Utafiti kutokana na kinachohisiwa na maradhi yatokanayo na ulaji wa kuku wa kisasa, napenda kuwaondoa hofu Watanzania wote, hakuna madhara yanayopthibitishwa kisayansi yanayotokana na ulaji wa kuku na mayai ya kisasa yanayopelekea kuota maziwa kwa wanaume au ndevu kwa wanawake.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!